MSANII CHEGE AKANUSHA MADAI YA KUVAA HIRIZI STEJINI

Msanii  kutoka katika kundi la Wanaume Family Chege Chigunda amejitokeza na kukanusha tetesi zilizoenea kuhusu picha yake anayoonekana amevaa kitu kinachofanana na hirizi katika mkono wake wa kushoto.Msanii huyo kutoka kundi la TMK amewashukia kwa ukali waandishi waliosambaza uvumi huo nakuweka wazi  kuwa alichokua amekivaa sio hirizi  bali ni kitu alivaa katika msiba wa msanii Mez B.

"Ushamba+roho mbaya+uandishi bila kusomea ni hatari sana hahaaahahahahahhaa eti waandishi magumashi wanadai nimevaa hirizi hahahhaaaaa hii tulivaa juzi dodoma siku ambayo alifariki msanii mwenzetu marehemu Mez B,msiwe vimbele mbele"

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele