Posts

Showing posts with the label news

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

Kijana Wa Miaka 26 Aeleza Alivyomzidi Naibu Gavana Wa Kaunti Ya Mombasa

Image
Joto la siasa linapamba moto wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Hivi sasa wanasiasa wengi wapo mbioni kujipigia debe wakijiandaa kuenda katika mchujo ili wapate tiketi ya chama ambacho watakua nacho kwenye debe ifikapo Agosti 8. Katika chama cha Jubilee ,   ni wagombea wawili tu ambao watakua wanapigani tikiti   ya chama hicho kuwania nyadhifa ya useneta wa kaunti ya Mombasa, naibu wa gavana wa kaunti ya Mombasa, bi Hazel Katana na bwana Abuubakar   Swabir .   Abuubakar ambaye anajipigia   upato kumpiku bi Hazel , amesema ya kwamba kuna vigezo vitano ambavyo vinampa   ujasiri wa yeye kumuangusha bi Hazel . ‘Huu ni wakati wa mageuzi, wananchi wamechoka na uongozi uliopo ndio maana watu wanataka watu wapya kabisa na ukiangalia mpinzani wangu, yeye si mgeni wa siasa kwa hivyo sioni kama ataweza kuwa kipenzi cha wengi kwa hilo….’ ‘Isitoshe, mwenzangu amekua katika serikali ya kaunti tangu kuanza kwa mfumo wa ugatuzi. Kwa miaka yote minne hi...

Joho Aandikia Serikali Barua

Image
Katika siku za hivi karibuuni, wanasiasa   na viongozi mbalimbali wannaompinga gavana wa Mombasa,   Ali Hassan   Joh o akiwemo rais Uhuru Kenyatta wamekua wakidai ya kwamba gavana huyo amefuja bilioni 40 ambazo ndio jumla ya mgao kwa kaunti ya Mombasa kutoka kwa serikali kuanzia mwaka wa 2013 hadi sasa. Baada ya kutoa kauli yake kuhusu swala hilo akidai ya kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea takriban shilingi bilioni   16 ( kshs 16, 396, 501, 522)   tu kutoka serikali kuu, gavana Joho ameandikia barua hazina ya taifa akiomba waweke wazi   kauli isiyo ya ukweli ya rais Kenyatta na vyombo vya habari inayosema kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea jumla ya shilingi bilioni 40 tangu kuanza kwa ugatuzi. Vilevile gavana Joho ameomba salio lililobakia ili kutimiza bilioni 40 ( Kshs 23, 603, 498, 478 ) kama inavyodaiwa kutumwa kwa serikali ya kaunti ya Mombasa mara moja.

Upinzani Uache Unafik, Asema Rais Uhuru Kenyatta

Image
Rais Uhuru Kenyatta amesema ya kwamba chama cha Jubilee ndio chama pekee ambacho kinapaswa kuongoza nchi hii. Akiongea katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika uwanja wa Tononoka , rais Uhuru alisema ya kwamba Jubilee ni chama ambacho kiliundwa kwa nia ya kuunganisha wananchi kwa nia ya kuwafanyia wananchi kazi ili kufanya miradi na maendeleo   ambayo yataboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Uhuru alisisitiza ya kwamba Jubilee pekee ndio suluhisho la maendeleo kwa wakaazi wa pwani kwani mirandi   iliyofanya serikali ya Jubilee kwa wapwani haikuwahi kufanywa na serikali zilizotangulia. Akitoa mfano wa   maendeleo yaliyofanyika katika eneo la pwani, rais Uhuru alisema ya kwamba tangu serikali yake iingine uongozini, imewapatia wananchi 200,000 hati miliki za mashamba katika   eneo la pwani tu   katika mda wa miaka minne ambayo amekua uongozini. ‘Tukiomba kura hatukulia lakini tulikua tunajua ya kwamba wapwani wamed...

Asilimia 99 Ya Wapwani Ni Wafuasi Wa Jubilee - Gedion Mung’aro

Image
M’bunge wa   eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Mh Gideon Mung’aro ambaye anapania kugombania ugava wa kaunti ya Kilifi kwa tikiti ya chama cha Jubilee amesistiza ya kwamba wapwani hawajiungi katika chama cha jubilee bali ni miongoni wa waanzilishi wa chama hicho na takriban asilimia   99 ya wapwani ni wafuasi wa Jubilee. Akiongea hayo katika mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee katika uwanja wa Tononoka uliofanyika hapo jana , Mh Gideon Mung’aro amesema ya kwamba eneo la pwani ni moja ya ngome kuu za   chama cha Jubilee na ana uhakika ya kwamba chama hicho kitajizolea kura za wapwani takriban asilimia 99 katika uchaguzi ujao. Bwana Mung’aro amesistiza ya kwamba   chama cha Jubilee ndio chama ambacho kimekua na utendakazi mzuri ndio maana viongozi wengi wamekua wakihama kutoka vyama vingine na kujiunga katika chama hicho katika siku za hivi karibuni.

Fat S Afunguka Kuhusu Mziki, Kuuza CD, Mayai Na Diss Ya Dogo Richie

Image
Wiki hii msanii Fat S ameongelewa sana baada ya kusemekana ya kwamba katika siku za hivi karibuni amekua akionekana akiuza mayai katika kivukio cha Likoni. Kelvin Jilani / Mtu Bei alifanikiwa kumpata Fat S na wakawa na mahojiano ambayo Fast S alifunguka mengi kuhusu yeye mziki na biashara zake. Katika mahojiano hayo,   Fat S alifunguka na kueleza ni jinsi gani amekua akiifanya biashara yake ya kuuza CD pale Ferry na inamuingizia pesa kiwango gani. ‘Unajua mimi ni msanii   na mimi ni kioo cha jamii. Kila kitu ninachofanya hua nafanya kwa ajili ya kufunza jamii, kwa hio ple ninapo uza Cd ferry naonyesha jamii ya kwamba nategemea kazi yangu na kipaji change ndio kinanilipa. Mimi sifanyi   mziki ubishow bali nafanya kama biashara. ‘ Fat S amesema huku akisema ya kwamba wale wasanii wengi ambao wamekua wakimcheka ndio ambao hawana lolote kwani ni njaa na kukosa pesa ndio wanajua ‘Msanii anayejua analofanya hawezi akaingia studio na kutoa pesa zake akaimb...