Kijana Wa Miaka 26 Aeleza Alivyomzidi Naibu Gavana Wa Kaunti Ya Mombasa
Joto la siasa linapamba moto wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Hivi sasa
wanasiasa wengi wapo mbioni kujipigia debe wakijiandaa kuenda katika mchujo ili
wapate tiketi ya chama ambacho watakua nacho kwenye debe ifikapo Agosti 8.
Katika chama cha Jubilee,
ni wagombea wawili tu ambao watakua wanapigani tikiti ya chama hicho kuwania nyadhifa ya useneta wa
kaunti ya Mombasa, naibu wa gavana wa kaunti ya Mombasa, bi Hazel Katana na
bwana Abuubakar Swabir. Abuubakar ambaye anajipigia upato kumpiku bi Hazel, amesema ya kwamba
kuna vigezo vitano ambavyo vinampa
ujasiri wa yeye kumuangusha bi Hazel.
‘Huu ni wakati wa mageuzi, wananchi wamechoka na uongozi
uliopo ndio maana watu wanataka watu wapya kabisa na ukiangalia mpinzani wangu, yeye
si mgeni wa siasa kwa hivyo sioni kama ataweza kuwa kipenzi cha wengi kwa
hilo….’
‘Isitoshe, mwenzangu amekua katika serikali ya kaunti tangu
kuanza kwa mfumo wa ugatuzi. Kwa miaka yote minne hio, hakuna maendeleo
aliyofanyia wananchi huku mashinani. Nadhani wana,Jubilee na watu wa Mombasa kwa ujumla wanataka viongozi wachapa
kazi si wale ambao wanapotea na kusahau kwamba wananchi wanangojea maendeleo na kuonekana tu wakati wa uchaguzi.
‘Nilitangaza nia yangu kugombania useneta miaka miwili
iliyopita na nimekua mashinani kwa mda mrefu nikiuza sera mashinani. Tofauti na mwenzangu
ambaye ni juzi tu ndio alitangaza nia
yake baada ya kuhama chama pinzani cha ODM.’
‘Sio kwamba nina ubaguzi wa kijinsia ila tangu jadi, si
Mombasa tu, wala Kenya ila Africa kwa ujumla tumekua na ugumu wa kuchagua
kiongozi wa kike na ukizingatia hilo basi utaona ya kwamba nina nafasi kubwa
kumpiku mwenzangu bila pingamizi…..
‘Nina ushawishi na wafuasi mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu. Mimi ndio muanzilishi wa Muungano wa vyuo vikuu pwani almaaruf
Coast University Colleges STudents Organisation ambayo niliiianzisha mnamo 2005.
Toka mda huo hadi sasa nimekua nikijihusisha pakubwa na mambo mbalimbali na wanafunzi wa vyuo hivyo
basi ninaamini ya kwamba nina wafuasi wengi vijana ukizingatia ya kwamba
takriban aslimia 80 ya wapiga kura ni vijana na wengi wao wapo katika vyuo vikuu..
Abuu ambaye alikua mgombeaji pekee kutoka
Mombasa aliyepewa fursa ya kuzungumza katika mkutano wa wawaniaji wa nyadhfa
mbalimbali mkoani pwani kupitia chama cha Jubilee uliofanyika katika eneo la
wildwaters. Mkutano ambao ulihudhuriwa na naibu wa rais wa Kenya, Mh. William
Samoei Ruto anaamini ya kwamba fursa hio inaonyesha ni jinsi gani ameweza kujiongezea
umaarufu na kukubali si kwa wananchi tuu bali hata kwa viongozi.
Abuubakar senAtor tukop amoja
ReplyDeleteAbuubakar senAtor tukop amoja
ReplyDeleteKwaujasiri na ubusara wa Abuubakar Senator.asilimia 99%amepita Moja niya Allah
ReplyDeleteHata Mimi Jubilee tuko pamoja
ReplyDelete