Posts

Showing posts with the label Entertainment

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

Mashabiki Wawaweka Roho Juu Dizzle Na Dogo Richie

Image
Baada ya kufanya vizuri kwa wimbo KIFAA, ambao Dizzle alimshirikisha hitmaker wa Mziki Majanga , hatimaye wawili hao wameachia video hio ambayo ilikua imesubiriwa kwa hamu na gamu. Kulingana na wawili hao ni kwamba hawakua na nia ya kufanyia video wimbo huo lakini mashabiki ndio waliowaskuma kufanya hivyo. 'Baada ya kuachia KIFAA tu, nilikua nikiulizwa kila siku kama nitaachia lini video yake. Nikapuuza mwanzoni lakini mskumo kutoka kwa mashabiki ulizidi kwani idai ya wanaouliza swali hilo ikawa inaongezeka nikaona sina budi ila kuwapa wanachotaka kwa sababu mwisho wa siku huu mziki nafanyia mashabiki, na nafaa kuwapatia wanachohitaji .' Alielezea Dizzle wakati akitambulisha rasmi video hio iliyoongozwa na Ricky Bekko wa BigDreams . Itazame hapa...

Hiki Ndicho Alichokifanya Baada Ya Kutimuliwa Studio

Image
Angekua na moyo mwepesi basi hata tusingewahi kumsika kwani   kilichomtokea katika jaribio lake la kwanza kufanya mziki kingemkatisha tama ila kwa kua alikua na malengo ya juu hakutetereka ila aliogeza ujasiri na moyo zaidi wa kufikia malengo yake. Adily Tozy alianze kupenda mziki tangia akiwa mtoto. Miaka miwili iliyopita Adily ndipo alipoona ya kwamba wakati mwafaka wa kuanza mziki rasmi umewadia. Akajizoazoa akiwa amejihami na mashairi kuenda studio afanye mawili matatu. Baada ya kupitishwa huku na kule kwa mda kiasi hatimaye alionana na   producer ambaye alimuandalia beat ya wimbo na kumpa akajitayarishe kurekodi. Alirudi studio baada ya wiki mbili na akabaahatika kupata mda mzuri na producer wake. Baada ya kuwa studio kwa zaidi ya takrriban masaa mawili wakijaribu kuandaa wiimbo wake wa kwanza, producer aliona ya kwamba msanii huyo likua hawezi kabisa na akaamua kumtoa nje ya studio na kumrudishia pesa zake na kumwambia   asiwahi kurudi tena katika st...

Cannibal Azungumzia Video Inayomuonyesha Akiwa Mlevi Chakari

Image
Siku ya Jumapili msanii Ralph Masai almaaruf Cannibal ambaye anagombania nyadhfa ya MCA Mtopanga ward alikua gumzo mitandaoni baada ya kuzaa kwa video iliyomuonyesha amelewa chakara. Ni video ambaye ilimfanya akashifiwe kwa sana. Wengi wakisema ya kwamba amejidhalilisha na amekosea kufanya kitendo kama hicho haswa ukizingatia ya kwamba anataka kua kiongozi , si wa vijana tu bali jamii nzima. Hatimaye Cannibal amefunguka na kuongea kuhusu kipande cha video hicho…  ‘Ukiskia ya kwamba siasa ni mchezo mchafu usidhani ni msemo tu. Ile video ni mimi ukweli, ila ni ya miaka sita nyuma, kitambo sana hata mimi ilinishtua kuipata mtandaoni siku ile. Tulifanya uchunguzi na kujua ya kwamba watu waliohusika kusambaza video ile ni wapinzani wangu ambao wanagombani nyadhfa ninayogombania pia.’ Cannibal amesema na kuongezea ya kwamba wapinzani wake wameingia mashinani na kujua ya kwamba yeye ndio kipenzi cha watu na hawana nafasi ya kumpiku ndio maana wakaamua kutumia njia chafu ili kum...

Aeleza Alichokipata Baada Ya Kuachia Video Kali

Image
Hisia Zangu ndio wimbo uliomtambulisha Mr Dawa katika soko la mziki na baadae msanii huyu alimshirikisha Dogo Richie katika kazi yake mpya ya LEOLEO. Mr Dawa ambaye alifanya track zaidi ya kumi mwanzoni ila hakuna aliyoiachia kwa kua aliona kazi hizo zilikua na viwango vya chini sana amedai ya kwamba  sasa ndio safari yake ya mziki imeanza rasmi. Mr Dawa ameyasema hayo baada ya kuachia video hio ambayo kulingana na yeye imemfungulia milango mingi katika sana katika biashara ya mziki. ‘Kufanya video nzuri ni muhimu sana na kunasaidia msanii kuweza kujijengea jina. Hisia Zangu ilikua track nzuri sana, ilichezwachezwa katika vyombo vya habari lakini haikufikia nilipo kua natarajia ifike lakini hii LEOLEO imefanya vizuri zaidi kwa sababu ina video nzuri .’ Mr   Dawa amesema huku akifunguka zaidi na kusema ya kwamba malengo yake ni kuweza kuwa na jina kubwa na si Afrika Mashariki tu wala Afrika tu bali dunia nzima. ‘Nataka nijijenga mpaka jina Mr Dawa linap...

Kundi Linalojihusisha Na Mziki, Uhamasisho na Biashara Kwa Vijana

Image
NewLife Music   si kundi tu la mziki bali pia ni shirika linalojihusisha kuhamasisha vijana kuishi maisha yenye muelekeo katika jamii. Waanzilishi wa kundi hili, Kally D na Baracka J.O hawafanyi mziki wa injili tu ila wanahubiri amani haswaa wakati huu nchi inapoelekea kufanya uchaguzi. Katika kuhubiri kwao, wanaowalenga sana ni vijana kwani hao ndio hutumika sanasana na wanasiasa na bila uhamasisho mzuri husababisha madhara makubwa si kwa vijana wenyewe tu bali kwa nchi nzima kwa ujumla. ‘ Kimziki   kwa sasa Kally D ameachia video yake ya NISHIKE na inaendelea kufanya vizuri na kuanzia mwezi ujao tutakua tunatayarisha video ya wimbo mmoja wangu. ’ Ameeleza Baracka J.O ambaye ameendelea kusema ya kwamba wanajihusisha na biashara ya mavazi na wako na clothingline   ( New Life Music -   NLM) ambayo wanaipangia kuifanyia uzinduzi mkubwa hivi karibuni. ‘ Tunakaribisha wasanii wenzetu wa injili wajiunge nasi. Atakayetuma maombi atakaguliwa kulingana na ...

Fat S Afunguka Kuhusu Mziki, Kuuza CD, Mayai Na Diss Ya Dogo Richie

Image
Wiki hii msanii Fat S ameongelewa sana baada ya kusemekana ya kwamba katika siku za hivi karibuni amekua akionekana akiuza mayai katika kivukio cha Likoni. Kelvin Jilani / Mtu Bei alifanikiwa kumpata Fat S na wakawa na mahojiano ambayo Fast S alifunguka mengi kuhusu yeye mziki na biashara zake. Katika mahojiano hayo,   Fat S alifunguka na kueleza ni jinsi gani amekua akiifanya biashara yake ya kuuza CD pale Ferry na inamuingizia pesa kiwango gani. ‘Unajua mimi ni msanii   na mimi ni kioo cha jamii. Kila kitu ninachofanya hua nafanya kwa ajili ya kufunza jamii, kwa hio ple ninapo uza Cd ferry naonyesha jamii ya kwamba nategemea kazi yangu na kipaji change ndio kinanilipa. Mimi sifanyi   mziki ubishow bali nafanya kama biashara. ‘ Fat S amesema huku akisema ya kwamba wale wasanii wengi ambao wamekua wakimcheka ndio ambao hawana lolote kwani ni njaa na kukosa pesa ndio wanajua ‘Msanii anayejua analofanya hawezi akaingia studio na kutoa pesa zake akaimb...

Otile Brown Aeleza Kwa Hasira Kilichompelekea Kujitoa DreamLand Music

Image
Katika mda wa wiki mbili sasa, msanii Otile Brown amekua akigonga vichwa vyaa habari baada ya kubainika ya kwamba kumekua na ugomvi kati yake na manager wake Dr Eddie baada ya Eddie kuzitoa video zote za msaniii huyo katika mtandao wa Youtube . Na hapo  jana asubui, Otile Brown aliweza kutangaza rasmi kupitia mitandao ya kijamii ya kwamba amejitoa katika management hio. Kasssim Mbui wa PiliPili FM alifanikiwa kufanya mahojiano na msanii huyo ili kujua ni kipi haswaa kilichojiri hadi kupelekea msanii huyo kufanya maamuzi hayo. ‘Nimekua nikitumia pesa zangu kuji,market kazi zangu. Kuna vitu alikua anastahili afanye lakini hakua akifanya. Alikua anafaa anilipie nyumba lakini nilikua najilipia mwenyewe. Baada ya ugomvi nlimtafuta tusuluhishe lakini amekua akikata simu zangu na kutoshika. Nimejaribu kumpigia zaidi ya mara mia mbili. Upande wa hela kuna mkataba kila mtu ana kile anachochangia na kila mtu ana asilimia yake ya mgao ambayo anapaswa kupata kipato kinachoingia....