Aeleza Alichokipata Baada Ya Kuachia Video Kali
Hisia Zangu ndio
wimbo uliomtambulisha Mr Dawa katika
soko la mziki na baadae msanii huyu alimshirikisha Dogo Richie katika kazi yake mpya ya LEOLEO.
Mr Dawa ambaye alifanya track zaidi ya kumi mwanzoni ila
hakuna aliyoiachia kwa kua aliona kazi hizo zilikua na viwango vya chini sana amedai ya
kwamba sasa ndio safari yake ya mziki imeanza rasmi. Mr Dawa ameyasema hayo baada ya kuachia video hio ambayo kulingana
na yeye imemfungulia milango mingi katika sana katika biashara ya mziki.
‘Kufanya video nzuri
ni muhimu sana na kunasaidia msanii kuweza kujijengea jina. Hisia Zangu
ilikua track nzuri sana, ilichezwachezwa katika vyombo vya habari lakini
haikufikia nilipo kua natarajia ifike lakini hii LEOLEO imefanya vizuri zaidi kwa sababu ina video nzuri.’ Mr
Dawa amesema huku akifunguka zaidi na kusema ya kwamba malengo yake
ni kuweza kuwa na jina kubwa na si Afrika
Mashariki tu wala Afrika tu bali
dunia nzima.
‘Nataka nijijenga mpaka jina
Mr Dawa linapotajwa watu wawe
wanajua ni nani anafanya kama tu vile Nelson
Mandela. I just want to be a big brand.’ Ndivyo alivyomalizia msaa
huyo.
Itazame video hio ambayo imempa matumaini ya
kuteka soko la mziki hapa.
I love the song n the video..Keep up Mr dawa.your star has started shining.aim the galaxy.
ReplyDeleteshikilia Hapo hapo
ReplyDelete