Posts

Showing posts with the label Videos

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

Mashabiki Wawaweka Roho Juu Dizzle Na Dogo Richie

Image
Baada ya kufanya vizuri kwa wimbo KIFAA, ambao Dizzle alimshirikisha hitmaker wa Mziki Majanga , hatimaye wawili hao wameachia video hio ambayo ilikua imesubiriwa kwa hamu na gamu. Kulingana na wawili hao ni kwamba hawakua na nia ya kufanyia video wimbo huo lakini mashabiki ndio waliowaskuma kufanya hivyo. 'Baada ya kuachia KIFAA tu, nilikua nikiulizwa kila siku kama nitaachia lini video yake. Nikapuuza mwanzoni lakini mskumo kutoka kwa mashabiki ulizidi kwani idai ya wanaouliza swali hilo ikawa inaongezeka nikaona sina budi ila kuwapa wanachotaka kwa sababu mwisho wa siku huu mziki nafanyia mashabiki, na nafaa kuwapatia wanachohitaji .' Alielezea Dizzle wakati akitambulisha rasmi video hio iliyoongozwa na Ricky Bekko wa BigDreams . Itazame hapa...

Susumila Alilia Mapenzi Mwezi Mmoja Kabla Kufunga Ndoa Tena (Video)

Image
Ikiwa bado mwezi mmoja tu kabla msanii Susumila kuuasi ukapera, amekutana na Timmy T Dat ambaye kwa pamoja wamefanya bongea la video la wimbo OYOO (Nipende) ambapo wanaonekana kulilia  mapenzi. Ni video iliyoandaliwa na Ricky Bekko wa BigDreams. Itazame hit hio mpya hapa chini...

Aeleza Alichokipata Baada Ya Kuachia Video Kali

Image
Hisia Zangu ndio wimbo uliomtambulisha Mr Dawa katika soko la mziki na baadae msanii huyu alimshirikisha Dogo Richie katika kazi yake mpya ya LEOLEO. Mr Dawa ambaye alifanya track zaidi ya kumi mwanzoni ila hakuna aliyoiachia kwa kua aliona kazi hizo zilikua na viwango vya chini sana amedai ya kwamba  sasa ndio safari yake ya mziki imeanza rasmi. Mr Dawa ameyasema hayo baada ya kuachia video hio ambayo kulingana na yeye imemfungulia milango mingi katika sana katika biashara ya mziki. ‘Kufanya video nzuri ni muhimu sana na kunasaidia msanii kuweza kujijengea jina. Hisia Zangu ilikua track nzuri sana, ilichezwachezwa katika vyombo vya habari lakini haikufikia nilipo kua natarajia ifike lakini hii LEOLEO imefanya vizuri zaidi kwa sababu ina video nzuri .’ Mr   Dawa amesema huku akifunguka zaidi na kusema ya kwamba malengo yake ni kuweza kuwa na jina kubwa na si Afrika Mashariki tu wala Afrika tu bali dunia nzima. ‘Nataka nijijenga mpaka jina Mr Dawa linap...

Azidisha Mbwembwe Baada Ya Kutoka Mafichoni

Image
Ni mwezi jana tu ndio msanii Professa Nasha aliweza kuachia kazi yake mpya baada ya kua mafichoni kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja baada ya kufumaniwa na mke wa mwanasiasa maarufu hapa pwani. Stori hio iko >> HAPA. Baada ya kurudi rasmi katika mziki, Professa Nasha ameamua ni kazi baada ya kazi kwani baada ya mwezi tu tayari ameandaa video mpya. ‘Nilikua nimewamiss mashabiki wangu na najua walikua wanakosa sana kazi nzuri kutoka kwangu lakini hio ni zamani kwa sababu nimerudi kuwaridhisha na nawaahidi kuwapa kazi nzuri bila kuchoka. Naelewa ya kwamba si rahisi kurudi nilipokua baada ya kimya cha mwaka mmoja lakini najibidisha kwa ajili ya mashabiki wangu.’ Nasha amesema hayo wakati alipokua anazindua video yake mpya ya ULIENDA WAPI iliyoandaliwa na DreamLand Music . Kua wa kwanza kuitanza video hiyo hapa chini....

Baada Ya Kufumaniwa Na Mke Wa Waziri, Ajitoa Mafichoni Kwa Mara Ya Kwanza Na Kueleza Yaliyotokea

Image
Mwaka wa 2015, Profesa Nasha alikua mmoja wa wasanii ambao walikua wanafanya vizuri kutoka eneo la pwani.   Wimbo wake wa POLE ulikua unachezwa sana katika vituo vya redio na ilipofika Januari 2016 , Nasha   akaachia wimbo mpya kwa jina MOTOKAA   ambao alikua amekamilisha kutayarisha video yake akisubiri   muongozaji amalize editing ndio aiachie baadae. Alichokua hajui ni kwamba video hio ingekwama na maisha yake kubadilika kwani alipatikana na mkosi ambao nusura auliwe. Profesa Nasha alifumaniwa akiwa na bibi ya waziri mmoja katika serikali ya   Kenya. Ni tukio ambalo lilimuacha na majeraha mabaya sana kwani aliangukia kipigo cha mbwa kutoka kwa walinzi wa waziri huyo na alipopata nafasi alitoroka, si hotelini mle tu bali ilibadilisha makao na kuenda mafichoni. ‘Kusema ukweli mimi sikuwahi kujua kua Yule alikua bibi ya mtu kwa sababu hakuwahi kuniambia. Tukio la kufumaniwa halikua rahisi kwangu kwani sikupewa nafasi ya kujieleza na nilipo...

Baada Ya Mziki Ni Majanga, Kaa La Moto Naye Aibuka Na MZIKI NI MATANGA

Image
Kaa La Moto naye ameibuka na wimbo alioshirikiana na Young Njita pamoja na mwanadada Wandia ambao wameonekana ni kana kwamba wanaunga mkono kauli ya Dogo Richy ya kwamba sanaa ya mziki katika eneo la Pwani limejaa shida na changamoto nyingi tu. Mziki umekua matanga wengi hatuna huzuni, hatuna uhuru labda Raila na Kibaki show hawakupi na wakikupa hawakulipi...uliza Sango mjini mipango labda wa kando wanagonja tufe waje kuleta michango …   ni baadhi ya mashairi ya wimbo huo ambao umeandaliwa video kali sanana director mashuhuri kutoka mjini Malindi, Marvin Y. Brudas . Ni video ambayo imetayarishwa katika mandhari tofauti na mazoea ya video zingine za kizazi kipya kwani ilitayarishwa katika jangwa na ubunifu mzuri wa maigiuzo. Itazame video hio ya mkali huyo wa hiphop katika Afrika Mashariki  aliyomshirikisha Young Njita ambaye anaonekana kuteka na kutawala soko la katika kaunti ya Kilifi.

CHIKUZEE AUNDA KUNDI LA MZIKI

Image
Msanii Chikuzee ni mmoja kati ya wasanii tajika kutoka kanda ya pwani ya Kenya. Waakati alipoachia collabo mbili na msanii Susumila mashabiki wengi walitamani sana wawili hao waungane na kuwa kundi moja ila uhusiano wao haukuduma sana kuanzia 2015 wawili hao walianz kua na tofauti baina yao. CNew naye alikua pamoja na msanii Fat S   na 35% katika kundi lao la RBeez ,   enzi hizo CNew alikua akijiita Njemba Boy .   Pia nalo ni kundi ambalo lilikuja vunjika baadae. Miaka imesonga sasa na wawili hao, Chikuzee na CNew katika siku za hivi karibuni wameonekana wakiwa na ukaribu sana na wameweka wazi ya kwamba, pamoja na Producer B.I wamekuja pamoja na kuunda kundi kwa jina DOSSARI INTERNATIONAL. ‘Tumeunda kundi na mtindo wetu wa mziki unaitwa TamTam Flevaz . Si kwamba ni kundi ambalo linatufunga sana bali kila mtu bado ana uhuru wa kufanya solo projects zake lakini tukiwa pamoja ndio Dossari International . Kuna kazi nyingi ambazo tayari tushazikamilis...

AWAACHA WATU HOI KWA KUJIBADILISHA

Image
Msanii kutoka Malindi, Beka Boy amepandisha joto katika anga za mziki na kuteka nyoyo za wengi baada ya kubadilisha style yake ya mziki. BekaBoy alianza mziki akiwa mdogo sana na kwa kua alikua na talanta kubwa aliweza kusajiliwa katika kundi la bango la Sea Waves Band. Akiwa SeaWaves aliweza kutunga nyimbo kama vile NITALIA ambayo ni moja kati ya nyimbo zilizotokea kupendwa sana kutoka kwa band hio. Akiwa katika band hio ya bango, alijiingiza pia katika mziki wa kizazi kipya ila kwa kushirikishwa tu na baadhi ya wanamziki wa hophop ili awafanyie chorus kwani sauti yake ya dhahabu imetokea kupendwa sanaaa. Jinsi   umri unavyopanda ndivyo kipaji chake kilivyokua kikiongezeka kwa ari na bidii aliyokua nayo na akaona katika band aliyoko hatumii kipaji chake vilivyo ndipo akaamua kuingia mzimamzima katika mziki wa kizazi kipya. Kama volcano vile, kazi yake ya kwanza ameonyesha jinsi alivyo na uzoefu wa kuimba na kwamba yeye ni mwanamziki kamili kwa sababu wimbo huo w...