AWAACHA WATU HOI KWA KUJIBADILISHA



Msanii kutoka Malindi, Beka Boy amepandisha joto katika anga za mziki na kuteka nyoyo za wengi baada ya kubadilisha style yake ya mziki. BekaBoy alianza mziki akiwa mdogo sana na kwa kua alikua na talanta kubwa aliweza kusajiliwa katika kundi la bango la Sea Waves Band. Akiwa SeaWaves aliweza kutunga nyimbo kama vile NITALIA ambayo ni moja kati ya nyimbo zilizotokea kupendwa sana kutoka kwa band hio.
Akiwa katika band hio ya bango, alijiingiza pia katika mziki wa kizazi kipya ila kwa kushirikishwa tu na baadhi ya wanamziki wa hophop ili awafanyie chorus kwani sauti yake ya dhahabu imetokea kupendwa sanaaa. Jinsi  umri unavyopanda ndivyo kipaji chake kilivyokua kikiongezeka kwa ari na bidii aliyokua nayo na akaona katika band aliyoko hatumii kipaji chake vilivyo ndipo akaamua kuingia mzimamzima katika mziki wa kizazi kipya.
Kama volcano vile, kazi yake ya kwanza ameonyesha jinsi alivyo na uzoefu wa kuimba na kwamba yeye ni mwanamziki kamili kwa sababu wimbo huo wa NIKO LOW una utunzi wa hali ya juu na sauti alivyoitoa ni lazma utataka kuskiza wimbo huo tena na tena. Wimbo huo ambao uliotayarishwa na Producer Sango pia umeandaliwa video kali sana…kali sana na muongozaji Marvin Y Brudas. Kabla nimalize hamu ya kazi hio kwa kusema wengi wacha nikupe fursa ya kujishuhudia kazi hio kali hapa chini…

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele