Posts

Showing posts from February, 2017

Baada Ya Kukaa Korokoroni Kwa Wiki Mbili, Ability Wa Wasojali Band Aeleza Yaliyojiri

Image
Ability ambaye ni mmoja wa kundi ya Wasojali Band ameeleza yaliyotokea hadi yeye kutupwa korokoroni kwa mda wa wiki mbili. Ability alitiwa mbaroni siku Februari 10 katika eneo la Mingira, Garsen wakati walipokua wanaelekea kupiga show Hola . ‘Ilikua siku ya Ijumaa na tulikua tunaelekea Hola kwa show yetu. Tulipofika katika roadblock ya Mingira, Garsen tukafanyiwa search na tukaambiwa tutoe vibali vyetu. Nilipotoa yangu wakaniambia ya kwamba ID yangu ni fake na wakaniweka katika ulinzi .’ Ability ameeleza. ‘Nilipokuja Kenya kutoka Tanzania nilikua hat sijafikisha miaka 18. Katika kupigapiga kazi nikaambiwa ya kwamba huenda nikatiwa mbaroni kwa kua sina kitambulisho. Aliyenieleza hayo akaniambia nikimpa hela flani ataniletea kitambulisho. Kwa kua mimi ni mgeni na skua najua kwamba kuna njia maalum ya kupata kitambulisho, nilipeana hela na baada ya siku mbili nikaletea kitambulisho nikajua hio issue nishamaliza. Ability amesimulia huku akiongeza na kusema ya kwamba ye

Hiki Ndicho Kitakachotokea Katika Kivukio Cha Mtongwe Kuanzia Ijumaa Hii

Image
Shirika la huduma za ferry limetangaza ya kwamba kivukio cha Mtongwe kitaanza kutumika tena kuanzia siku ya Ijumaa , Februari 24 . Kuanza kutumika tena kwa kivukio hicho cha Mtongwe kutaleta afueni kwa zaidi ya abiria 30,000 kila siku. Kivukio cha Mtongwe kitaanza tena huduma zake baada ya   kufanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi milioni 6 baada ya serikali kuondoa ferry mbili zilizokua zikihudumu katika kivukio hicho mnamo 2012. Msimamizi mkuu kwa huduma za ferry, Bakari Gowa ameeleza ya kwamba   moja kati ya ferry tano zinazotumika katika kivukio cha Likoni itatumika katika kivukio hicho cha Mtongwe . ‘Moja kati ya MV LIKONI na MV KWALE itakua inahudumu katika kivukio cha Mtongwe . Kwa kuanzia, huduma za ferry Mtongwe zitakua wakati wa msongamano, alafu ratiba ya huduma itabadilika kulingana na jinsi huduma hizo zitakavyopokelewa na huenda zikaanza kufanya kazi siku nzima.’   Bwana Gowa ameeleza   huku akiendelea na kusema ya kwamba anaamini ya kwamba kurudi kw

Je, PiliPili FM ‘Walimkanyagia’ Interview Akothee?

Image
Siku moja kabla ya tamasha lake la ‘pre valentine’ msanii anayeaminiwa kua msanii tajiri zaidi nchini Kenya, Akothee alikua anastahili kuwa na mahojiano katika kituo cha redio cha PiliPili FM katika kipindi cha MwakeMwake Live na mtangazaji Gates Mgenge ila inasemekana ya kwamba msanii huyo alikatazwa kuingia katika studio za PiliPili FM hata baada ya kufika katika   kituo hicho cha redio . Je ni kipi kilichosababisha msanii huyo kutohojiwa hata baada ya kufika PiliPili FM? Kulingana na producer wa kipindi hichho, Clavery Khonde ni kwamba mahojiano yalikua yamepangwa kufanyika kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa moja jioni, tamati mwa kipindi hicho lkini msanii huyo akafika dakika tano kabla kipindi hicho kuisha… ‘Si kwamba Akothee aliringiwa au alibaniwa lakini ni kwa sababu alikuja kuchelewa na ilikua vigumu kufanya mahojiano. Alikuja dakika tano kabla kipindi kuisha na kulingana na sheriia ya kituo   huo ndio mda ambao mtangazaji hu,signout .’ ‘Akothee ni

Nimetungia Wasanii Wengi Hit Songs Bila Kuitisha Hata Senti - Producer AMZ

Image
Producer mkali na mkongwe kutoka studio za Tempoz, Amz wa Leo amejipiga kifua katika swala zima la uandishi na kusema kwamba sio katika upishi wa beat tu pekee bali hata katika swala zima la utunzi yuko vizuri saana. Kulingana na Amz ni kwamba ameshawahi kutunga hits nyingi sana ambazo zimewaacha mdomo wazi wasanii wenyewe anaowaandikia. "Nina uwezo wa kukuandikia wimbo hadi ujiulize nilichokifikiria ni kipi na wazo la wimbo limetokea wapi .” Amz amesema kuwa kuna hits nyingi kubwa zilizo na mkono wake ila hajalipisha hata senti. "Nikijiskia kuandikia mtu naandika tu bila kutarajia malipo wala credits zozote. Hua ni hisia fulani hunijia na hunisumbua mpaka hujipata nimepigia msanii yeyote simu aje nimuandikie wimbo ndio nijiskie sawa....." Amz amesema huku akidinda kutaja baadhi ya ngoma ambazo zina utunzi wake.

Pastor Aeleza Kwanini Alim'beba Mgongoni Kalonzo Musyoka

Image
Kuanzia siku ya Jumapili, picha ya aliyewahi kua makamu wa rais , Kalonzo Musyoka akiwa amebebwa mgongoni na pastor flani ilizua gumzo sana katika mitandao ya kijamii. Haikua imebainika ni kwanini walifanya kitendo kile na ilikuaje mpaka ikafikia pale. Siku ya Jumatatu, katika kipindi cha MegaBreakfast, Baraka FM , watangazaji Billy Miya na Diana Tangut aka Presenter 001 waliweza kumtafuta pastor   huyo, Pastor Daniel Idaturi wa Jesus Winning Soul Ministry ili aeleze haswaa kilichokua kinatendeka katika picha ile. ‘Katika kuhubiri nilikua nahubiri pale   Yesu Kristo alipoagiza mwanafunzi wake amlee punda na kumwambia ya kkwamba atakapoulizwa ni nani anayehitaji punda yule basi asema   ni Bwana wangu ndiye anayetaka punda. Kalonzo Musyoka alikua Yesu na mimi nikawa Punda. ’ Pastor Daniel alieleza.   Je alipoamriwa kumpanda pastor mgongoni, Kalonzo aliipokeaje amri hio? Ni waumini ndio walimshabikia kumpata pastor au ilikuaje? Na je ni kweli baada ya ibada pastor Daniel

Berry Black Awakashif Mashabiki, Wasanii Na Washikadau Wa Mziki Pwani

Image
Ni mmoja kati ya wasanii kutoka nchini Tanzania ambao wameweza kujulikana sana Afrika Mashariki. Akiwa na mwenzake Berry White wakiwa na kundi lao la 2Berry , walihit sana na wimbo NATAKA KUA NAWE a mbao ulitayarishwa na Producer Shirko   ambaye ni producer kutoka Mombasa. Kufanya kazi kwa wawili hao hakukuishi hapo kwani karibu ntimbo zote za Berry Black zimeandaliwa na Producer Shirko ambaye ndiye producer anayetayarisha nyimbo za Yamoto Band. Hapo jana, usiku wa Alhamisi, katika ukumbi wa Dans Lounge, katika tamasha la Celebrity Thursday, Berry Black aliwatolewa mapovu na kuwakashif mashabiki kutoka Mombasa na washikadau katika sanaa ya mziki kutoka Mombasa kwa kukosa ku,support watu na kazi za nyumbani. ‘Nyinyi watu wa Mombasa ham,support watu wenu. Shirko alipokua anaongea hapa hamkua munampigia makofi lakini mimi nimeshika mic munanipigia makofi. Hizo nyimbo munazo zishabikia na kuniambia niimbe yeye ndio amezitengeneza. Yamoto Band kufika walipofika ni m

Baada Ya Kufumaniwa Na Mke Wa Waziri, Ajitoa Mafichoni Kwa Mara Ya Kwanza Na Kueleza Yaliyotokea

Image
Mwaka wa 2015, Profesa Nasha alikua mmoja wa wasanii ambao walikua wanafanya vizuri kutoka eneo la pwani.   Wimbo wake wa POLE ulikua unachezwa sana katika vituo vya redio na ilipofika Januari 2016 , Nasha   akaachia wimbo mpya kwa jina MOTOKAA   ambao alikua amekamilisha kutayarisha video yake akisubiri   muongozaji amalize editing ndio aiachie baadae. Alichokua hajui ni kwamba video hio ingekwama na maisha yake kubadilika kwani alipatikana na mkosi ambao nusura auliwe. Profesa Nasha alifumaniwa akiwa na bibi ya waziri mmoja katika serikali ya   Kenya. Ni tukio ambalo lilimuacha na majeraha mabaya sana kwani aliangukia kipigo cha mbwa kutoka kwa walinzi wa waziri huyo na alipopata nafasi alitoroka, si hotelini mle tu bali ilibadilisha makao na kuenda mafichoni. ‘Kusema ukweli mimi sikuwahi kujua kua Yule alikua bibi ya mtu kwa sababu hakuwahi kuniambia. Tukio la kufumaniwa halikua rahisi kwangu kwani sikupewa nafasi ya kujieleza na nilipopata nafasi nilikimbia n