Baada Ya Kukaa Korokoroni Kwa Wiki Mbili, Ability Wa Wasojali Band Aeleza Yaliyojiri
Ability ambaye ni mmoja wa kundi ya Wasojali Band ameeleza yaliyotokea hadi yeye kutupwa korokoroni kwa mda
wa wiki mbili.
Ability alitiwa mbaroni siku Februari 10 katika
eneo la Mingira, Garsen wakati
walipokua wanaelekea kupiga show Hola. ‘Ilikua siku ya Ijumaa na tulikua
tunaelekea Hola kwa show yetu. Tulipofika katika roadblock ya Mingira, Garsen tukafanyiwa search na
tukaambiwa tutoe vibali vyetu. Nilipotoa yangu wakaniambia ya kwamba ID yangu
ni fake na wakaniweka katika ulinzi.’ Ability
ameeleza.
‘Nilipokuja Kenya
kutoka Tanzania nilikua hat
sijafikisha miaka 18. Katika kupigapiga kazi nikaambiwa ya kwamba huenda
nikatiwa mbaroni kwa kua sina kitambulisho. Aliyenieleza hayo akaniambia
nikimpa hela flani ataniletea kitambulisho. Kwa kua mimi ni mgeni na skua najua
kwamba kuna njia maalum ya kupata kitambulisho, nilipeana hela na baada ya siku
mbili nikaletea kitambulisho nikajua hio issue nishamaliza. Ability amesimulia huku akiongeza na
kusema ya kwamba yeye alikua anajua ya kwamba yuko sawa tu hata siku hio ya kutiwa mbaroni
alishtuka sana kuambiwa ya kwamba stakabadhi aliyokua nayo ilikua ghushi.
Baada ya kuwekwa katika ulinzi mkali, Ability
alifikishwa mahakamani jumanne
iliyofuata ili kusomewa mashtaka na kurudishwa korokoroni. Baada ya kufikishwa
kortini mara tatu na kukaa korokoroni kwa wiki mbili, Februari
21, kulingana na alivyojitetea Ability alinusurika kifungo cha miaka mitano na baada yake akahukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya Kshs. 20,000 na kuruhusiwa kutengeneza stakabadhi sahihi. ‘Nashkuru meneja wangu, Athman Baba alishuhulikia kuachiliwa
kwangu na sasa nashuhulika kupata vibali rasmi vya kuwa hapa Kenya. Yani kule
ndani si kwa kukaa, ni kugumu sana na kulinifanya nijue umuhimu wa kua huru.’
Ability amemamalizia.
Pole bro na usirudie tena hata ukihamia nchi nyengine usijaribu kutumia njia ya mkato
ReplyDelete