Posts

Showing posts with the label Gossip

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

Cannibal Azungumzia Video Inayomuonyesha Akiwa Mlevi Chakari

Image
Siku ya Jumapili msanii Ralph Masai almaaruf Cannibal ambaye anagombania nyadhfa ya MCA Mtopanga ward alikua gumzo mitandaoni baada ya kuzaa kwa video iliyomuonyesha amelewa chakara. Ni video ambaye ilimfanya akashifiwe kwa sana. Wengi wakisema ya kwamba amejidhalilisha na amekosea kufanya kitendo kama hicho haswa ukizingatia ya kwamba anataka kua kiongozi , si wa vijana tu bali jamii nzima. Hatimaye Cannibal amefunguka na kuongea kuhusu kipande cha video hicho…  ‘Ukiskia ya kwamba siasa ni mchezo mchafu usidhani ni msemo tu. Ile video ni mimi ukweli, ila ni ya miaka sita nyuma, kitambo sana hata mimi ilinishtua kuipata mtandaoni siku ile. Tulifanya uchunguzi na kujua ya kwamba watu waliohusika kusambaza video ile ni wapinzani wangu ambao wanagombani nyadhfa ninayogombania pia.’ Cannibal amesema na kuongezea ya kwamba wapinzani wake wameingia mashinani na kujua ya kwamba yeye ndio kipenzi cha watu na hawana nafasi ya kumpiku ndio maana wakaamua kutumia njia chafu ili kum...

Fat S Aacha Kuuza CD Na Kuanza Kuuza Mayai Ferry

Image
Msanii Fat S amekua gumzo kwa mda mrefu kwa biashara yake ya kujiuzia CD katika kivukio cha Likoni. Wengi wamekua wakisema ya kwamba shida nyingi na kukosa hela ndiko kunakomsukuma msanii huyo kujiuzia CD zake ferry jambo ambalo amelikana akidai ya kwamba kuuza CD ferry kunampa kipato kikubwa zaidi ya biashara yeyote anayoweza kufikiria kufanya kwa sababu kwa siku hawezi kukosa kuingizi takriban Kshs. 20,000 mfukoni. Ila katika siku za hivi karibuni Fat S amezua kizungumkuti. Hio ni baada ya kuonekana akiuza mayai badala ya cd katika kivukio hicho. Kwa mda wa takriban wiki mbili sasa, msanii huyo ameonekana kutupilia mbali kuuza CD na kukita kuuza mayai yakuchemshwa. Baada ya kupata picha kadhaa za msanii huyo akiendelea na biashara hio,meza yetu ya habari imejaribu kumfikia msanii huyo ila amekua hapokei simu zetu wala kujibu hata ujumbe mmoja kati ya nyingi alizotumiwa.

Susumila Kufunga Ndoa Mwezi Wa Aprili

Image
Kando na kufanya kazi nyingi na kubwa mwaka wa 2016 , moja ya vitu vilivyoongelewa sana kumhusu ni kutalakiana na aliyekua mkewe, Kibibi Salim ambaye walikua wameoana kwa miezi 11 tu.  Miezi   mitano sasa baada ya Susumila kutalakiana na muigizaji Kibibi Salim ambaye walikua wamejaaliwa mtoto mmoja, mdokezi wetu wa kuaminika ametudokezea ya kwamba Susumila anajipanga kufunga pingu za maisha mwezi wa Aprili.   Mdokeni wetu ambaye ni rafiki wa karibu sana wa msanii huyu amedinda kumfichua   bibi harusi mtarajiwa ila ametudokezea tu ya   kwamba mrembo huyo aliyeteka moyo wa Susumila ni mtoto wa mwanasiasa mmoja tajika kutoka eneo la pwani na harusi ya wawili hao haitafanyika nchini Kenya . ‘Zile safari nyingi ambazo Susumila amekua akisafiri zimekua si za matembezi tu bali ni za matayarisho ya harusi yao. Harusi yenyewe imepangwa kuhudhuriwa na watu 35   tu. Watu wote hao watagharamiwa usafiri na malazi kkatika nchi ambayo kutafanyika harusi h...

Producer Khalid Atiwa Mbaroni

Image
Baada ya vuta nikuvute ya siku mbili kati ya msanii PDay na Producer Khalid, drama kati ya wawili hao haijaishia mtandaoni tu bali imesababisha Producer Khalid kutupwa korokoroni. Malumbano yote hayo yalianza hapo jana wakati PDay aliandika katika katika ukurasa wake wa facebook ya kwamba Producer Khalid amedinda kumpatia video aliyomtayarishia akidai ya kwamba mabinti waliotumika na msanii huyo katika video hio ni wabovu. Wakati Khalid akijibu madai hayo, alisema ya kwamba msanii huyo ni mtu asiyekua na shukrani. Pday naye amemgeuzia kibao producer huyo akisema ya kwamba Khalid ndiye wa kwanza kukosa shukrani kwani hata yeye ndiye aliyemsaidia kupata loan yake ya kwanza kwa 'mzee Rajab'. Kufikia mida ya saa kumi na robo alasiri, kumeanza kuenea uvumi ya kwamba producer Khalid ametiwa mbaroni, ili kuthibithisha uvumi huo, Gates Mgenge katika kipindi cha MwakeMwake, PiliPili Fm amempigia simu PDay ambaye ameeleza yaliyojiri... 'Khalid ni kakangu wa mda mrefu...

Is Archy Kawere Cheating With An Upcoming Singer?

Image
Katikati siku za hivi karibu  kumekua na minong'ono ya kwamba huenda mke wa mwanamziki mkongwe hapa pwani Archy Kawere,   akiwa anacheza mechi za nje na msanii chipukizi anayekua kwa kasi,  hit maker wa NI WEWE,  Iddi Singer. Uvumi huo umeletwa na ukaribu ambao wawili hao wamekua nao katika siku za hivi karibuni kwani wamekua wakionekana katika mikahawa mbalimbali wakiwa pamoja. Isitoshe, wamewahi kufanya photoshoot pamoja mara kadhaa na hata mwishoni mwa wiki jana, siku ya Jumamosi, wawili hao waliandamana wakati msanii huyo alipokua anaenda katikati shooting ya kipindi cha Mseto EA ambako walionekana katika mapozi tatanishi   na pia kuitana majina ya mapenzi na kubembelezana kama vile Bae na beib mitandaoni. Nikimuuliza  Archy  kuhusu  uvumi huu amejibu  na kusema ya kwamba nimuulize swali hilo mwishoni mwa wiki.Naye Iddi nilipomuuliza kuhusu swala hilo alisema ya kwamba hajibu swali lolote isipokua maswali yanayohusu mzi...