Producer Khalid Atiwa Mbaroni
Baada ya vuta nikuvute ya siku mbili kati ya msanii PDay na Producer Khalid, drama kati ya wawili hao haijaishia mtandaoni tu bali imesababisha Producer Khalid kutupwa korokoroni.
Malumbano yote hayo yalianza hapo jana wakati PDay aliandika katika katika ukurasa wake wa facebook ya kwamba Producer Khalid amedinda kumpatia video aliyomtayarishia akidai ya kwamba mabinti waliotumika na msanii huyo katika video hio ni wabovu.
Wakati Khalid akijibu madai hayo, alisema ya kwamba msanii huyo ni mtu asiyekua na shukrani. Pday naye amemgeuzia kibao producer huyo akisema ya kwamba Khalid ndiye wa kwanza kukosa shukrani kwani hata yeye ndiye aliyemsaidia kupata loan yake ya kwanza kwa 'mzee Rajab'.
Kufikia mida ya saa kumi na robo alasiri, kumeanza kuenea uvumi ya kwamba producer Khalid ametiwa mbaroni, ili kuthibithisha uvumi huo, Gates Mgenge katika kipindi cha MwakeMwake, PiliPili Fm amempigia simu PDay ambaye ameeleza yaliyojiri...
'Khalid ni kakangu wa mda mrefu, hata unakumbuka mimi ndio nilimtambulisha kwako Gates. Na si kwako tu, Khalid nimemtambulisha kwa watu wengi sana katika hii industry ila sijui ni kitu gani kimebadilika hadi yeye anataka kunidhulumu. Mimi nadai haki yangu, akinilipa elfu zangu kumi basi sina kesi naye. Amewekwa ndani dakika chache zilizopita. Watu wake waje wamsaidie anilipe pesa zangu tumalizane na anafaa ajue ya kwamba mzee hatemewi mate.' PDay ameleeza akithibithisha ya kwamba ni kweli Producer Khalid yuko mikononi mwa polisi.

Comments
Post a Comment