Posts

Showing posts from January, 2017

Sina Tatizo Na Susumila Wala TK2, Na Haya Ndiyo Nimepanga Kuyafanya- KIGOTO

Image
Baada ya msanii Mswazi Masauti kuachana na management ya Swa RnB ameonekana akiwa na ukaribu sana na msanii Kigoto ambaye pia aliachana na management ya Number 1 Records ya Producer TK2 . Wawili hawa wamejitokeza na kusema kwamba wanafanya kazi pamoja ila haijabainika iwapo kushikana kwao ni kufanya collabo tu au wameunda kundi. Katika mahojiano na Kelvin Jilani (MTU BEI) , Masauti ameeleza mpangilio wao wa kufanya kazi na kile ambacho mashabiki wanapaswa kutarajia kutoka kwao. Kwa upande mwengine Kigoto naye amefunguka ya kwamba wamekua wakipata mskumo kutoka kwa mashabiki ambao wamekua wakilalamika ya kwamba wamekimya sana bila kuachia kazi yoyote kwa mda mrefu. Vilevile Kigoto ameeleza uhusiano wake na aliyekua producer na manager wake, Producer Tk2 , akijibu swali ya kipi kilichomfanya atengana na ‘mlezi’ wake huyo na iwapoo bado wanaweza kufanya kazi pamoja. Katika swali lengine ambalo lilikua limewekwa mezani na shabiki, Kigoto ameeleza maoni yake baada ya Susu

AWAACHA WATU HOI KWA KUJIBADILISHA

Image
Msanii kutoka Malindi, Beka Boy amepandisha joto katika anga za mziki na kuteka nyoyo za wengi baada ya kubadilisha style yake ya mziki. BekaBoy alianza mziki akiwa mdogo sana na kwa kua alikua na talanta kubwa aliweza kusajiliwa katika kundi la bango la Sea Waves Band. Akiwa SeaWaves aliweza kutunga nyimbo kama vile NITALIA ambayo ni moja kati ya nyimbo zilizotokea kupendwa sana kutoka kwa band hio. Akiwa katika band hio ya bango, alijiingiza pia katika mziki wa kizazi kipya ila kwa kushirikishwa tu na baadhi ya wanamziki wa hophop ili awafanyie chorus kwani sauti yake ya dhahabu imetokea kupendwa sanaaa. Jinsi   umri unavyopanda ndivyo kipaji chake kilivyokua kikiongezeka kwa ari na bidii aliyokua nayo na akaona katika band aliyoko hatumii kipaji chake vilivyo ndipo akaamua kuingia mzimamzima katika mziki wa kizazi kipya. Kama volcano vile, kazi yake ya kwanza ameonyesha jinsi alivyo na uzoefu wa kuimba na kwamba yeye ni mwanamziki kamili kwa sababu wimbo huo wa NI

Ajipanga Kua Bingwa Wa HipHop Pwani

Image
Donrich  ni rapper anayechipuka na anajipigia upato na kuamini ya kwamba mwaka huu yeye ndio msanii wa hiphop kutoka pwani ambaye atatamba zaidi.   Donrich  amesema ya kwamba ana imani kubwa sana na ushairi wake na style yake kwani anaongea vitu ambavyo vipo mitaani na ni mambo ambayo kila mtu anaweza ku,relate nayo. Akitoa mfano wa wimbo wake mpya ambao amezungumzia  jinsi alivyoishi vizuri na kukubalika kuliko  hapo awali  kwa sababu mafanikio ameyapata na maisha yanamuendea vizuri. ‘’Nilipokua jana sipo nilipo leo na naamini kila mtu hua ana ndoto ya kupata mafanikio ili mbeleni asiwe kama alivyokua awali. Ni kitu ambacho kila mtu anaweza ku,relate nacho. ‘   Donrich  amesema hayo huku akisistiza ya kwamba yeye ndio msanii wa hiphop pekee wa kuangaliwa mwaka huu wakati alipokua anachia track yake mpya ambayo unaweza kuipata >> HAPA

ThrowBack Track... Totti & Sleem G Feat. Gates Mgenge- JUU JUU

Image
Mwaki ni 2012 ambapo Producer Totti japo alikua tayari ashaonyesha uwezo wake wa kutayarisha mziki kupitia hits kama vile ' Maria' ya Ali B na Nyota Ndogo alikua hajazoeleka sana kama msanii. Wakati huu ndio pia alikua ameshirikiana na wasanii kadhaa kama vile Johnny skani , K-lama,Kavalier   na wasanii wengine katika wimbo wa We Run M.S.A na collabo nyengine na Kidis katika wimbo 'Tujirushe' . Wakati huu pia Sleem G naye ndio alikua anafanya solo projects zake baada ya kuvunjika kwa kundi lao la Outta Limits huku mtangazaji Gates Mgenge naye alikua anatamba na kipindi chake cha  'MashavMashav' akiwa na mtangazaji mkongwe Donde Samora huku akiwa anatamba katika viwanja vya burudani kama Dj,  hypeman na vilevile MC. Watatu hao kwa pamoja waliingia studio na kufanya track kwa jina JUU JUU , japo haikua wahi kuhit sana ila ilipata kuchezwa kwa kiasi cha haja katika vituo kadhaa vya redio na kumbi za burudani. Track yenyewe iko >> HAPA

DJ Ivory Asema Asiwahi Kuhusishwa Tena Katika Tuzo Zozote Za Pwani. Kulikoni?

Image
Mshindi wa tuzo mbili,  Dj Ivory ametangaza kwambaa  hataki tena kuhusishwa katika tuzo zozote kutoka hapa pwani. Kupitia ukurasa wake wa facebook, Ivory amesema ya kwamba baada ya kufikiria kwa mda mrefu sasa anaona ni wakati mwafaka wa yeye kusitisha kushiriki katika tuzo zozote kutoka Mombasa na Pwani kwa ujumla ili kuwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao djs wanaochipuka. Nikimhoji zaidi baadae, nilimuuliza iwapo kama madai ya kwamba tuzo za Mombasa/Pwani hua hazina uwazi wala usawa ndio kumeachangia yeye kufanya maamuzi hayo… ‘ Hapana. Nina imani sana na Awards za hapa nyuumbani na mimi hua naona ziko fair kabisa ila wale wenye kusema hivyo ni kwa sababu ya hao kukosa kujiamini.’ Vilevile, Ivory ambaye ni dj katika kipindi cha MashavMashav, Pwani FM amesema ya kwamba mwaka huu ni fursa nyingine tena ya kujiendeleza na kupanua kazi zake kwani kampuni yake ya HHD Entertainment imepanga kuinua mziki na wasanii wa Mombasa na Pwani kwa ujumla  kwa kiwango kikubwa sana mwa

Je Ni Kweli Kundi La MAFIOSO Lilivunjika Baada Ya Kushinda Tuzo?

Image
MAFIOSO ni kundi ambalo liliweza kushinda tuzo ya kundi lenye bidii zaidi katika tuzo za Coast Music Awards mwishoni mwa 2016. Kuwekua na tetesi ya kwamba kundi hilo lilivunjika tu baada ya kushinda tuzo hio. Tetesi hizo zilianza kuzagaa wakati mmoja wa kundi hilo , Pukka Pisces kuanza kuonekana peke yake mara nyingi kinyume na alivyokua amezoeleka kuonekana akiwa na mwenzake Ruksy. Dalili nyengine ya kuvunjika kwa kundi hilo ni ilijitokeza pale Pukka alipoachia video akiwa peke yake bila mwenzake Ruksy. 'Ni kweli watu wamekua wakiniona peke yangu bila Ruksy ila si eti kundi limevunjika. Ruksy alisafiri, yupo Ujerumani na familia yake kwa sasa ndio maana hata kwa hii video hayupo lakini kundi bado lipo imara sana.' Pukka amesema hayo akikana tetesi hizo. Video hio ya MAFIOSO iiliyoandaliwa na muongozaji X-ANTONIO inaenda kwa jina LOVE ME, ambayo wimbo ulitayarishwa na ma,producer wawili, Morbizz nna Producer BeatsBoy unaweza kuitazama hapa chini.

Brown Mauzo Awahusisha Diamond Na Akothee Katika Video Yake Mpya

Image
Collabo yake na mkali wa bongofleva, msanii AliKiba imemfanya kutambulika pakubwa katika tasnia ya mziki Afrika Mashariki . Nchini   Tanzania , uhusiano wa Brown Mauzo na AliKiba unachukuliwa kama vile wa Harmonize na boss wake Diamond Platnumz , hii ni baada ya AliKiba kutangaza ya kwamba Brown ni mmoja wa wasanii ambao wako katika management yake. Katika kazi yake mpya Brown ameshangaza wengi baada ya kuachia video ambayo inaonekana ya kwamba amem,copy hasimu wa boss wake, Diamond Platnumz kwa ku,copy idea ya video ya ‘ Salome ’ ambayo alishirikishwa Rayvanny na vilevile Brown ameipa kazi hio jina la utata ( Apotee)  kwani limefanana na msanii Akothee ambaye ana uhusiano wa karibu na Diamond na pia ni mpenzi wa zamani wa Brown. Itazame video yenyewe hapa chini…

Msanii Wakike Aporwa Mali Na Msanii Wakiume

Image
Siku hizi unaambiwa Mziki ni Majanga  ila katika hayo majanga ya mziki, wanamziki wanapata majanga ya mapenzi pia. Msanii wa kike kutoka Mombasa, Smin Shally alipata majanga ya mapenzi kupitia mziki baada ya kutapeliwa mali yake na msanii wa kiume ambaye alikua ‘dume suruale’.   Smin Shally alijitosa katika uhusiano na mwanamziki mmoja kutoka hapa Kenya  mzima mzima. Kwa kua alikua amezama katika penzi zito la msanii huyo ambaye mfuko wake ulikua mtupu aliamua kumgharamia maisha ili angalau naye aishi maisha ya hadhi na huku bado akimgharamia kazi zake za mziki kwa hela yake. Kila uchao penzi lao lilikua likinawiri na Smin akawa anazidi kua muwazi na kumgharamikia zaidi mshikaji wake huyo kwa kua alikua anajua ya kwamba kifo ndicho kitakacho watenganisha tu. Akawa akiwekeza na kununua mali anaziandikisha kwa jina la mpenzi wake msanii, kumbe alikua anajichimbia kisima bila kujua. Jamaa aliamka sku moja tu akamwambia Smin ya kwamba hamtaki tena. Baada ya vuta nikuvute Smin ak

Fat S Afichua Kinachomsukuma Kuuza CD Zake Ferry.

Image
Msanii Fat S aka Mtoto Wa Nyanya kwa mda mrefu amekua akiwa kicheko kwa baadhi ya wasanii na  mashabiki kwa kile kinaonekana kama ‘kuhangaika’ . Sababu ya yeye kuonekana kuhangaika ni yeye kuonekana mda mwingi akiuza cd za mziki wake katika kivukio cha Likoni. Japo amekua kicheko na kejeli na kutumika kama mfano ya kua mziki ni mgumu hadi inabidi wasanii wengine wauze cd wenyewe barabarani, kama alivyoimba msanii Chikuzee katika wimbo wa MZIKI alioshirikishwa na Dodo Richy, Fat S hajawahi acha kuuza kazi zake katika kivukio cha Likoni. Hivi ni kwanini? Je ni kwamba hali ni ngumu sana na ndio njia aliyonayo pekee ya kujikimu au mauzo ni vipi? ‘Mimi ferry peke yake pananitosha kufanya biashara na kuendeleza familia yangu. Hata watu wakaungana zaidi ya elfu moja, watasema mpaka wachoke kwa sababu pale ferry ambapo panafanya watu wacheke sana kwa siku pananiingizia karibu Kshs.20,000 . Cd moja ni ksh.100. nikiuza cd kidogo kwa siku ni copy 200. Palepale ferry ndio pananifanya na

Blogger Madebe Aporwa!!

Image
Wanasema Nairobi ni jiji la wajanja na ukiwa mgeni wajanja na jiji watakukaribisha kwa kukupora. Blogger kutoka Mombasa ambaye alihamisha makaazi yake jijini Nairobi amepata mkosi wa kuporwa jijini humo. Madebe aliporwa nyumbani kwake wakati alipokua yupo kazini. Blogger huyo ambaye amekua akifuliwa na mfanyikazi huyo kwa mda aliingia mtegoni hapo jana kwa kumuacha mfanyikazi huyo peke yake nyumbani kwake huku akielekea kazi. Hio ilikua ni tofauti na kawaida yake ambayo alikua akifuliwa wakati yeye mwenyewe yupo nyumbani. Aliporudi jioni, alishanga kuona ya kwamba meko, laptop, na vitu vya matumizi katika jokovu lake havipo isipokua maji tu. Isitoshe, mfanyikazi huyo mwizi alichukua nguo zake zote na pesa zilizokua chumbani mwake. 'Nimewezwa kuwezwa yani. hata sijui nianzie wapi. Lakini ni sawa tu, yote ni ya Mungu. Lakoni stress yangu kubwa ni kwa laptop kwa sababu ni ya kazi na ina vitu vingi sana vya kampuni na wateja. Siju nifanyeje yani.' Ameeleza blogger huyo.

Mfanyibiashara TSS Afariki Dunia

Image
  Mfanyibiashara maarufu kutoka jijini Mombasa Tahir Sheik Said amefariki dunia. Akiongea na wanahabari, mwanawe Twahil ni kwamba marehemu amefariki katika hospitali ya Milpark Hospital, mjini Johannesburg, Afrika Kusini alipokua anaendelea na matibabu ambako alipelekwa December 15, 2016 kwa matibabu zaidi. Mwendazake alikua mfanyibiashara maarufu sana ambaye alikua ameekeza katika sekta ya usafiri, usagaji wa mahindi na ngano katika kaunti ya Mombasa na Lamu. Vilevile ni mmiliki wa moja ya jengo refu mjini Mombasa,TSS Towers.

Wynas Aachana Na TeeHits Na Kujiunga Na Record Label Mpya

Image
Nilimuorodhesha kama mmoja ya wasanii ambao huenda wakapasua mbarika sana mwaka huu wa 2017  >> HAPA . Hitmaker wa KITORIRO , Wynas ambaye amekua yupo chini ya uangalizi wa TeeHits inayomilikiwa na Producer Tee ameihama label hio na kujiunga na label nyengine. Wynas ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliachia wimbo wake wa NARINGA amejiunga rasmi na BigDreams ambayo ndio label inayomuangalia msanii Kush Tracey . 'Nimejiunga na BigDreams kwa sababu nimeona ni kampuni ambayo ina nia na uwezo wa kufanikisha ndoto zangu. Namshkuru sana Producer Tee kwa sababu amenitoa mbali na kunifikisha nilipo kwa sasa kwa sababu amekua kama mzazi kwangu ila lazima mtu apige hatua asonge mbele. Kulingana na ile mikakati tuliyopanga na BigDreams niko na imini sana ya kwamba tutafanikisha .' Wyna s ameeleza akithibithisha habari hizo. 'Wynas ni msanii ambaye ana,talent kubwa sana. Nimekua nikimfuatilia kwa mda mrefu sana na nliona ya kwamba nikimshika mkono tunaweza kufanya vi

Gavana Kingi Atangaza Msimamo Wake Baada Ya Kunyang'anywa Walinzi

Image
Gavana wa kaunti ya Kilifi, Amason Jeffah Kingi hatimaye ametoa kauli yake baada ya walinzi wake kuamrishwa kurudisha silaha na kurudi kambini. Akiongea na wanahabari, gavana huyo amesema ya kwamba usiku wa kuamkia Jumamosi, walinzi wanaolinda boma lake walichukuliwa na wale wanaomlinda yeye binafsi waliamrishwa kurudisha silaha siku ya Jumamosi na kurudi kambini. Gavana huyo alieleza ya kwamba hawakuelezwa sababu iliyopelekea serikali huchukua hatua hio ambayo imemfanyika yeye na gavana wa kaunti ya Mombasa, Hassan Ali Joho. Kingi ameeleza ya kwamba jambo hilo si mara ya kwanza kuwatokea wawili hao kwani serikali iliwafanyia hivyohivyo, yeye na gavana Joho baada ya uchaguzi mdogo wa Malindi. Kingi amesistiza ya kwamba, iwapo kungekua na sababu yoyote ya walinzi hao kutolewa basi wangefanyiwa heshima kwa kua hao ni viongozi wanaoendesha serikali na waelezwe sababu za hatua hio. 'Bado tunajiuliza maswali. Kuna njama gani ambayo imepangwa mpaka walinzi hawa wametol

Ana Uwezo Wa Kufanya Utake Kunyolewa Ukiangalia Michoro Yake Tu

Image
Akili ni nywele,  kila mtu ana zake na ubunifu na talanta ni vitu ambavyo kila mtu amejaaliwa kivyake.  Uchoraji ni moja ya kipaji ambacho mtu anaweza  akajaaliwa nacho, ila inahitaji ubunifu kutumia kipaji hiki ili mtu kuweza kua tofauti na wengine. Moses Kituwani, almaaruf   Msanii The Barber ana uwezo wa kufanya michoro kichwani, si kwa kutumia rangi au ‘tattoo’ ila kwa kunyoa nywele ili zitokeee kama mchoro aliobuni au anaotaka anayenyolewa. Kazi hii yake ya usanii wa kuvutia alianza mnamo 2009. Mwanzoni alikua mchorani stadi ila maisha yakawa hayamuendei vizuri kwa sababu sanaa ya uchorji picha haikua inamlipa vizuri. Ndio ikabidi atafute kazi ambayo itakua inamuingizia mtonyo wa kujikimu na mahitaji yake ya kila siku. Kazi aliyobahatika kupata ilikua ni kua ‘cashier’ katika salon moja mjini Mombasa . Wakati akiendelea na kazi hio alivutiwa na jinsi vinyozi wa pale walivyokua wakinyoa watu kwa style tofauti tofauti na akaanza kujifunza kunyoa. Kwa ubunifu wake na uzo