Blogger Madebe Aporwa!!

Wanasema Nairobi ni jiji la wajanja na ukiwa mgeni wajanja na jiji watakukaribisha kwa kukupora.
Blogger kutoka Mombasa ambaye alihamisha makaazi yake jijini Nairobi amepata mkosi wa kuporwa jijini humo.
Madebe aliporwa nyumbani kwake wakati alipokua yupo kazini. Blogger huyo ambaye amekua akifuliwa na mfanyikazi huyo kwa mda aliingia mtegoni hapo jana kwa kumuacha mfanyikazi huyo peke yake nyumbani kwake huku akielekea kazi. Hio ilikua ni tofauti na kawaida yake ambayo alikua akifuliwa wakati yeye mwenyewe yupo nyumbani.
Aliporudi jioni, alishanga kuona ya kwamba meko, laptop, na vitu vya matumizi katika jokovu lake havipo isipokua maji tu. Isitoshe, mfanyikazi huyo mwizi alichukua nguo zake zote na pesa zilizokua chumbani mwake. 'Nimewezwa kuwezwa yani. hata sijui nianzie wapi. Lakini ni sawa tu, yote ni ya Mungu. Lakoni stress yangu kubwa ni kwa laptop kwa sababu ni ya kazi na ina vitu vingi sana vya kampuni na wateja. Siju nifanyeje yani.' Ameeleza blogger huyo.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele