Posts

Showing posts with the label Music

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele

Image
Ukitaja wasanii ambao waliwahi kutamba kutoka eneo la pwani huwezi kukosa kumtaja Daddy Sele . Miaka ile ya 2008 alikua anatamba sana na wimbo wake wa Machungu na Ananipenda , wimbo ambao aliufanya na Fat S .  Wimbo wake wa Machungu , uliotayarishwa BC International ndio single yake kubwa ambayo ilimfanya atese sana katika anga za mziki baada ya kufanya track kama vile Badman , aliyokua ameifanya katika studio za Tabasamu Records ambayo haikuwahi kupata airplay nzuri. Kwa sasa, Daddy Sele ameacha kabisa mziki na kulingana na yeye ni kwamba yeye kufanya mziki basi itakua ni miujiza, aliongelea hilo >> HAPA. Kila siku ya alhamisi utakua unapata fursa ya kupata wimbo/video moja ya kitamboooo... unaweza ku,request katika eneo la ku,comment hapo chini. Download/Listen MACHUNGU >> HAPA

Baada Ya Kupata Ufadhili Mpya, WAKASI wamerudi Tena Katika Sanaa Na Hii Mpya

Image
Wakasi ni mandugu walofatana, Abubakar Kitole(Safa) na Robert Mwadzidze(Roy) kutoka Kilifi. Walianza safari ya mziki mwaka wa 2010 mjini Malindi studio ya Terrbyte . Wameshawahi kufanya nyimbo kadha lakini hazikufanya vizuri kwa sababu ya kukosa ubora wa kiwango cha chini cha nyimbo hizo. Licha ya kutoka kwenye familia yenye hadhi ya chini lakini wamejaribu kueneza ujumbe wenye umuhimu katika jamii. Wamewahi kupewa ufadhili fulani ambao haukudumu kwa muda kwa sababu haukua unamuelekeo mzuri wa kuwanufaisha lakini baadae mwaka wa 2015 ndio walipata na Joseph Lewa mmoja wa shirika linalo toa ufadhili kwa mambo ya kimaisha ya kila siku kama elimu, talanta, magojwa ambaye aliamua kujitolea kuanza kuwapa support na kuendeleza safafri yao ya mziki na kuwapa uwezo wa kufanya track hii mpya katika studio za  Tee Hits . Kua wa kwanza kupata wimbo mpya wa MAPENZI MATAMU >>; HAPA

Hiki Ndicho Queen Renee Alichorudi Nacho Kutoka Tour Yake Nchini Ujerumani

Image
Mwaka ukianza, Queen Renee ali,launch album yake ya KAMATA CHAMPAGNE baada ya kumaliza tour yake ya miezi mitatu nchini Ujerumani na Switzerland. Amekua akiachia project kila mwezi tangu Februari , kama si video basi ni audio kutoka kwa album yake hio kabla kuenda kwa tour nyengine ya mwezi mmoja kuanzia mwezi wa October. Queen Renee ametua nyumbani na amekuja na project mpya ikiwa bado ni muendelezo wa album yake hio ya KAMATA CHAMPAGNE. Kabla hata kuchezwa katika kituo chochote  ha redio, umebahatika kuwa kati ya watu wa kwanza kupata wimbo huo uliotayarishwa na Producer Akeem .. Ipate>> HAPA

Amshirikisha Kidis Katika Hii Mpya Baada Ya Kimya Cha Mwaka Mmoja

Image
Aliachia wimbo wake wa mwisho 2015 na baadae kukaa kimya. Si kwamba mziki ulikua umemshinda ila alikua anajitafta na kupanga mbinu za kujiweka vizuri katika ramani ya mziki. Baada ya kimya hicho, Babza amevunja ukimya na TUWAPIGE BAO , track ambayo amemshirikisha Kidis The Jembe na ni mkono wa Producer TK2, Number 1 Records . Kua Wa kwanza kuskia wimbo huo >> HAPA