Posts

Showing posts with the label Politics

Kwa Sasa Inapatikana Kwa www.machampalimedia.com

Image
Usipitwe na habari, matukio na vitu vingine vingi vipya vinapochipuka.Utaendelea kupata uhondo wote uliokua ukiupata humu ndani kupitia www.machampalimedia.com . Ni bora zaidi na vitengo vingi zaidi, usipitwe, bonyeza  >>  HAPA << uweze kuji,update.

Kijana Wa Miaka 26 Aeleza Alivyomzidi Naibu Gavana Wa Kaunti Ya Mombasa

Image
Joto la siasa linapamba moto wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Hivi sasa wanasiasa wengi wapo mbioni kujipigia debe wakijiandaa kuenda katika mchujo ili wapate tiketi ya chama ambacho watakua nacho kwenye debe ifikapo Agosti 8. Katika chama cha Jubilee ,   ni wagombea wawili tu ambao watakua wanapigani tikiti   ya chama hicho kuwania nyadhifa ya useneta wa kaunti ya Mombasa, naibu wa gavana wa kaunti ya Mombasa, bi Hazel Katana na bwana Abuubakar   Swabir .   Abuubakar ambaye anajipigia   upato kumpiku bi Hazel , amesema ya kwamba kuna vigezo vitano ambavyo vinampa   ujasiri wa yeye kumuangusha bi Hazel . ‘Huu ni wakati wa mageuzi, wananchi wamechoka na uongozi uliopo ndio maana watu wanataka watu wapya kabisa na ukiangalia mpinzani wangu, yeye si mgeni wa siasa kwa hivyo sioni kama ataweza kuwa kipenzi cha wengi kwa hilo….’ ‘Isitoshe, mwenzangu amekua katika serikali ya kaunti tangu kuanza kwa mfumo wa ugatuzi. Kwa miaka yote minne hi...

Cannibal Azungumzia Video Inayomuonyesha Akiwa Mlevi Chakari

Image
Siku ya Jumapili msanii Ralph Masai almaaruf Cannibal ambaye anagombania nyadhfa ya MCA Mtopanga ward alikua gumzo mitandaoni baada ya kuzaa kwa video iliyomuonyesha amelewa chakara. Ni video ambaye ilimfanya akashifiwe kwa sana. Wengi wakisema ya kwamba amejidhalilisha na amekosea kufanya kitendo kama hicho haswa ukizingatia ya kwamba anataka kua kiongozi , si wa vijana tu bali jamii nzima. Hatimaye Cannibal amefunguka na kuongea kuhusu kipande cha video hicho…  ‘Ukiskia ya kwamba siasa ni mchezo mchafu usidhani ni msemo tu. Ile video ni mimi ukweli, ila ni ya miaka sita nyuma, kitambo sana hata mimi ilinishtua kuipata mtandaoni siku ile. Tulifanya uchunguzi na kujua ya kwamba watu waliohusika kusambaza video ile ni wapinzani wangu ambao wanagombani nyadhfa ninayogombania pia.’ Cannibal amesema na kuongezea ya kwamba wapinzani wake wameingia mashinani na kujua ya kwamba yeye ndio kipenzi cha watu na hawana nafasi ya kumpiku ndio maana wakaamua kutumia njia chafu ili kum...

Joho Aandikia Serikali Barua

Image
Katika siku za hivi karibuuni, wanasiasa   na viongozi mbalimbali wannaompinga gavana wa Mombasa,   Ali Hassan   Joh o akiwemo rais Uhuru Kenyatta wamekua wakidai ya kwamba gavana huyo amefuja bilioni 40 ambazo ndio jumla ya mgao kwa kaunti ya Mombasa kutoka kwa serikali kuanzia mwaka wa 2013 hadi sasa. Baada ya kutoa kauli yake kuhusu swala hilo akidai ya kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea takriban shilingi bilioni   16 ( kshs 16, 396, 501, 522)   tu kutoka serikali kuu, gavana Joho ameandikia barua hazina ya taifa akiomba waweke wazi   kauli isiyo ya ukweli ya rais Kenyatta na vyombo vya habari inayosema kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea jumla ya shilingi bilioni 40 tangu kuanza kwa ugatuzi. Vilevile gavana Joho ameomba salio lililobakia ili kutimiza bilioni 40 ( Kshs 23, 603, 498, 478 ) kama inavyodaiwa kutumwa kwa serikali ya kaunti ya Mombasa mara moja.

Upinzani Uache Unafik, Asema Rais Uhuru Kenyatta

Image
Rais Uhuru Kenyatta amesema ya kwamba chama cha Jubilee ndio chama pekee ambacho kinapaswa kuongoza nchi hii. Akiongea katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika uwanja wa Tononoka , rais Uhuru alisema ya kwamba Jubilee ni chama ambacho kiliundwa kwa nia ya kuunganisha wananchi kwa nia ya kuwafanyia wananchi kazi ili kufanya miradi na maendeleo   ambayo yataboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Uhuru alisisitiza ya kwamba Jubilee pekee ndio suluhisho la maendeleo kwa wakaazi wa pwani kwani mirandi   iliyofanya serikali ya Jubilee kwa wapwani haikuwahi kufanywa na serikali zilizotangulia. Akitoa mfano wa   maendeleo yaliyofanyika katika eneo la pwani, rais Uhuru alisema ya kwamba tangu serikali yake iingine uongozini, imewapatia wananchi 200,000 hati miliki za mashamba katika   eneo la pwani tu   katika mda wa miaka minne ambayo amekua uongozini. ‘Tukiomba kura hatukulia lakini tulikua tunajua ya kwamba wapwani wamed...

Asilimia 99 Ya Wapwani Ni Wafuasi Wa Jubilee - Gedion Mung’aro

Image
M’bunge wa   eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Mh Gideon Mung’aro ambaye anapania kugombania ugava wa kaunti ya Kilifi kwa tikiti ya chama cha Jubilee amesistiza ya kwamba wapwani hawajiungi katika chama cha jubilee bali ni miongoni wa waanzilishi wa chama hicho na takriban asilimia   99 ya wapwani ni wafuasi wa Jubilee. Akiongea hayo katika mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee katika uwanja wa Tononoka uliofanyika hapo jana , Mh Gideon Mung’aro amesema ya kwamba eneo la pwani ni moja ya ngome kuu za   chama cha Jubilee na ana uhakika ya kwamba chama hicho kitajizolea kura za wapwani takriban asilimia 99 katika uchaguzi ujao. Bwana Mung’aro amesistiza ya kwamba   chama cha Jubilee ndio chama ambacho kimekua na utendakazi mzuri ndio maana viongozi wengi wamekua wakihama kutoka vyama vingine na kujiunga katika chama hicho katika siku za hivi karibuni.

Polisi Wapiga Breki Mkutano Wa Hadhara Wa ODM

Image
Chama cha ODM kimepigwa breki kufanya mkutano wa hadhara ambao ulikua umepangwa kufanyika hii leo katika uwanja wa Mvita. Kulingana na barua aliyoandikiwa mwenyekiti wa chama hicho tawi la kaunti ya Mombasa kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Makupa ni kwamba chama hicho kilikosa kuomba ruhusa ya kuandaa mkutano huo masaa 72 kabla ya   siku ya mkutano kama inavyostahili. Vilevile, mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee uliohudhuriwa na   Uhuru Kenyatta uliofanyika katika uwanja wa Tononoka pamoja na mkutano wa maombi wa prophet Owuor imetumia usalama mkubwa hivyo basi kupunguza uwezo wa polisi kupeana usalama katika mkutano mwengine wa hadhara. Kunyimwa kibali kwa mkutano huo ambao ulikua uongozwe na gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho ni hatua ambayo imeonekana kupunguza joto la kisiasa ambalo limekua linatarajiwa siku ya leo kwani kufanyika kwa wakati mmoja kwa mikutano ya vyama hivyo viwili pinzani kulikua   kunaonekana kama kupimana ngumu na kuonye...