Upinzani Uache Unafik, Asema Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta amesema
ya kwamba chama cha Jubilee ndio
chama pekee ambacho kinapaswa kuongoza nchi hii.
Akiongea katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama
hicho katika uwanja wa Tononoka, rais Uhuru alisema ya kwamba Jubilee ni chama ambacho kiliundwa kwa
nia ya kuunganisha wananchi kwa nia ya kuwafanyia wananchi kazi ili kufanya
miradi na maendeleo ambayo yataboresha
maisha ya mwananchi wa kawaida.
Uhuru alisisitiza
ya kwamba Jubilee pekee ndio
suluhisho la maendeleo kwa wakaazi wa pwani kwani mirandi iliyofanya serikali ya Jubilee kwa wapwani haikuwahi kufanywa na serikali zilizotangulia.
Akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika
katika eneo la pwani, rais Uhuru
alisema ya kwamba tangu serikali yake iingine uongozini, imewapatia wananchi 200,000 hati miliki za mashamba
katika eneo la pwani tu katika mda wa miaka minne ambayo amekua
uongozini.
‘Tukiomba kura
hatukulia lakini tulikua tunajua ya kwamba wapwani wamedhulumiwa na tukaona ni
sawa wapwani watekelezewe… wanasema ni haki yenu serikali kuwafanyia maendeleo
lakini mbona serikali zilizotangulia hazikufanya hivyo? Ni kwa sababu serikali
ya Jubilee ni serikali yenu ndio
maana inawatekelezea haki yenu.’ Rais Kenyatta
aliyasema hayo huku akieleza ya kwamba serikali yake imetumia zaidi ya kshs bilioni 30 katika ujenzi wa
barabara katika eneo la pwani.
Akimalizia, rais alisema ya kwamba wapinzani
waache unafiki na matusi kwani yeye ana simama kideti na kazi aliyofanya katika
miaka minne kazini sio kama baadhi ya magavana wa upinzani wanaojipiga kifua
wakati hawawezi eleza jinsi walivyotumia bilioni 40 zilizogawia kaunti zao
Comments
Post a Comment