Joho Aandikia Serikali Barua
Katika siku za hivi karibuuni, wanasiasa na viongozi mbalimbali wannaompinga gavana wa
Mombasa,
Ali Hassan Joho akiwemo rais
Uhuru Kenyatta wamekua wakidai ya kwamba gavana huyo amefuja bilioni 40 ambazo
ndio jumla ya mgao kwa kaunti ya Mombasa kutoka kwa serikali kuanzia mwaka wa 2013 hadi sasa.
Baada ya kutoa kauli yake kuhusu swala hilo akidai ya kwamba
serikali ya kaunti ya Mombasa
imepokea takriban shilingi bilioni 16 ( kshs 16, 396, 501, 522) tu kutoka serikali kuu, gavana Joho ameandikia
barua hazina ya taifa akiomba waweke wazi kauli isiyo ya ukweli ya rais Kenyatta na
vyombo vya habari inayosema kwamba serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea jumla
ya shilingi bilioni 40 tangu kuanza kwa ugatuzi.
Vilevile gavana Joho
ameomba salio lililobakia ili kutimiza bilioni 40 ( Kshs 23, 603, 498, 478) kama inavyodaiwa kutumwa kwa serikali ya kaunti
ya Mombasa mara moja.
Comments
Post a Comment