Asilimia 99 Ya Wapwani Ni Wafuasi Wa Jubilee - Gedion Mung’aro


M’bunge wa  eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Mh Gideon Mung’aro ambaye anapania kugombania ugava wa kaunti ya Kilifi kwa tikiti ya chama cha Jubilee amesistiza ya kwamba wapwani hawajiungi katika chama cha jubilee bali ni miongoni wa waanzilishi wa chama hicho na takriban asilimia  99 ya wapwani ni wafuasi wa Jubilee.
Akiongea hayo katika mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee katika uwanja wa Tononoka uliofanyika hapo jana, Mh Gideon Mung’aro amesema ya kwamba eneo la pwani ni moja ya ngome kuu za  chama cha Jubilee na ana uhakika ya kwamba chama hicho kitajizolea kura za wapwani takriban asilimia 99 katika uchaguzi ujao.
Bwana Mung’aro amesistiza ya kwamba  chama cha Jubilee ndio chama ambacho kimekua na utendakazi mzuri ndio maana viongozi wengi wamekua wakihama kutoka vyama vingine na kujiunga katika chama hicho katika siku za hivi karibuni.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele