Asilimia 99 Ya Wapwani Ni Wafuasi Wa Jubilee - Gedion Mung’aro
M’bunge wa eneo bunge
la Kilifi Kaskazini, Mh Gideon Mung’aro
ambaye anapania kugombania ugava wa kaunti ya Kilifi kwa tikiti ya chama cha
Jubilee amesistiza ya kwamba wapwani hawajiungi katika chama cha jubilee
bali ni miongoni wa waanzilishi wa chama hicho na takriban asilimia 99 ya wapwani ni
wafuasi wa Jubilee.
Akiongea hayo katika mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee katika uwanja wa Tononoka uliofanyika hapo jana, Mh Gideon Mung’aro amesema ya kwamba
eneo la pwani ni moja ya ngome kuu za
chama cha Jubilee na ana
uhakika ya kwamba chama hicho kitajizolea kura za wapwani takriban asilimia 99 katika uchaguzi ujao.
Bwana Mung’aro
amesistiza ya kwamba chama cha Jubilee ndio chama ambacho kimekua na
utendakazi mzuri ndio maana viongozi wengi wamekua wakihama kutoka vyama
vingine na kujiunga katika chama hicho katika siku za hivi karibuni.
Yunakenga yuyu Mung'aro be kisha
ReplyDelete