Polisi Wapiga Breki Mkutano Wa Hadhara Wa ODM



Chama cha ODM kimepigwa breki kufanya mkutano wa hadhara ambao ulikua umepangwa kufanyika hii leo katika uwanja wa Mvita.
Kulingana na barua aliyoandikiwa mwenyekiti wa chama hicho tawi la kaunti ya Mombasa kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Makupa ni kwamba chama hicho kilikosa kuomba ruhusa ya kuandaa mkutano huo masaa 72 kabla ya  siku ya mkutano kama inavyostahili. Vilevile, mkutano wa hadhara wa chama cha Jubilee uliohudhuriwa na  Uhuru Kenyatta uliofanyika katika uwanja wa Tononoka pamoja na mkutano wa maombi wa prophet Owuor imetumia usalama mkubwa hivyo basi kupunguza uwezo wa polisi kupeana usalama katika mkutano mwengine wa hadhara.

Kunyimwa kibali kwa mkutano huo ambao ulikua uongozwe na gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho ni hatua ambayo imeonekana kupunguza joto la kisiasa ambalo limekua linatarajiwa siku ya leo kwani kufanyika kwa wakati mmoja kwa mikutano ya vyama hivyo viwili pinzani kulikua  kunaonekana kama kupimana ngumu na kuonyeshana ubabe na umaarufu baina ya vyama hivyo

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele