Cannibal Azungumzia Video Inayomuonyesha Akiwa Mlevi Chakari

Siku ya Jumapili msanii Ralph Masai almaaruf Cannibal ambaye anagombania nyadhfa ya MCA Mtopanga ward alikua gumzo mitandaoni baada ya kuzaa kwa video iliyomuonyesha amelewa chakara. Ni video ambaye ilimfanya akashifiwe kwa sana. Wengi wakisema ya kwamba amejidhalilisha na amekosea kufanya kitendo kama hicho haswa ukizingatia ya kwamba anataka kua kiongozi , si wa vijana tu bali jamii nzima. Hatimaye Cannibal amefunguka na kuongea kuhusu kipande cha video hicho… 
‘Ukiskia ya kwamba siasa ni mchezo mchafu usidhani ni msemo tu. Ile video ni mimi ukweli, ila ni ya miaka sita nyuma, kitambo sana hata mimi ilinishtua kuipata mtandaoni siku ile. Tulifanya uchunguzi na kujua ya kwamba watu waliohusika kusambaza video ile ni wapinzani wangu ambao wanagombani nyadhfa ninayogombania pia.’ Cannibal amesema na kuongezea ya kwamba wapinzani wake wameingia mashinani na kujua ya kwamba yeye ndio kipenzi cha watu na hawana nafasi ya kumpiku ndio maana wakaamua kutumia njia chafu ili kumchafulia jina.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele