Msanii Wakike Aporwa Mali Na Msanii Wakiume
Siku hizi unaambiwa Mziki ni Majanga ila katika hayo majanga ya mziki, wanamziki wanapata majanga ya mapenzi pia.
Msanii wa kike kutoka Mombasa, Smin Shally alipata majanga ya mapenzi kupitia mziki baada ya kutapeliwa mali yake na msanii wa kiume ambaye alikua ‘dume suruale’. Smin Shally alijitosa katika uhusiano na mwanamziki mmoja kutoka hapa Kenya mzima mzima. Kwa kua alikua amezama katika penzi zito la msanii huyo ambaye mfuko wake ulikua mtupu aliamua kumgharamia maisha ili angalau naye aishi maisha ya hadhi na huku bado akimgharamia kazi zake za mziki kwa hela yake.
Kila uchao penzi lao lilikua likinawiri na Smin akawa anazidi kua muwazi na kumgharamikia zaidi mshikaji wake huyo kwa kua alikua anajua ya kwamba kifo ndicho kitakacho watenganisha tu. Akawa akiwekeza na kununua mali anaziandikisha kwa jina la mpenzi wake msanii, kumbe alikua anajichimbia kisima bila kujua. Jamaa aliamka sku moja tu akamwambia Smin ya kwamba hamtaki tena. Baada ya vuta nikuvute Smin akidhani pengine tu ni mzaha au ni hasira ya kitu flani alishanga akiambiwa atoke nyumbani humo, nyumba ambayo alikua ameijenga kwa jasho lake mwenyewe, akijaribu kupinga nndio akakumbushwa ya kwamba nyumba hio si yake kwa kua ilikua imeandikishwa kwa jina la msanii huyo wa kiume ambaye alikua mpenzi wake wa mda mrefu na sasa anamtimua.
Ndipo alipogudua makosa aliyofanya kwa kuingia mtegoni mwa tapeli huyo wa mapenzi ila alikua ashachelewa. Kati hali ya kupunguza uchungu wake, Smin ambaye pia ni mwanamitindo katika nchi ya Ujerumani aliingia studio pamoja na Dogo Richy na Muscador kutoka Congo na kufanya wimbo wakieleza uhalisia huo >>HAPA

Tatizo machampali watuachia ujumbe nusunusu.Msanii wa kiume sasa ndio nani.Malizia kazi bwana.
ReplyDelete