Gavana Kingi Atangaza Msimamo Wake Baada Ya Kunyang'anywa Walinzi


Gavana wa kaunti ya Kilifi, Amason Jeffah Kingi hatimaye ametoa kauli yake baada ya walinzi wake kuamrishwa kurudisha silaha na kurudi kambini.
Akiongea na wanahabari, gavana huyo amesema ya kwamba usiku wa kuamkia Jumamosi, walinzi wanaolinda boma lake walichukuliwa na wale wanaomlinda yeye binafsi waliamrishwa kurudisha silaha siku ya Jumamosi na kurudi kambini. Gavana huyo alieleza ya kwamba hawakuelezwa sababu iliyopelekea serikali huchukua hatua hio ambayo imemfanyika yeye na gavana wa kaunti ya Mombasa, Hassan Ali Joho.


Kingi ameeleza ya kwamba jambo hilo si mara ya kwanza kuwatokea wawili hao kwani serikali iliwafanyia hivyohivyo, yeye na gavana Joho baada ya uchaguzi mdogo wa Malindi. Kingi amesistiza ya kwamba, iwapo kungekua na sababu yoyote ya walinzi hao kutolewa basi wangefanyiwa heshima kwa kua hao ni viongozi wanaoendesha serikali na waelezwe sababu za hatua hio.
'Bado tunajiuliza maswali. Kuna njama gani ambayo imepangwa mpaka walinzi hawa wametolewa. Ikiwa ni kweli walinzi hawa wametolewa kwa sababu ya misimamo wetu na gavana Joho basi hawataregeshwa kwa sababu msimamo wangu hautabadilika kamwe na msimamo wa gavana Joho hautabadilika kamwe. If this is the price am going to pay for being in ODM, then so be it. I can not negotiate my being in ODM, being in ODM is priceless.'  Gavana huyo ameeleza huku akisistiza ya kwamba iwapo kuondolewa kwa walinzi wake ni njama ya kuyumbisha msimamo wake katika chama cha ODM basi ni heri akataftiwa sababu nyengine kwa sababu hatawahi kughairi wala kubadilisha msimamo wake katika chama hicho.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele