Ajipanga Kua Bingwa Wa HipHop Pwani
Donrich ni
rapper anayechipuka na anajipigia upato na kuamini ya kwamba mwaka huu
yeye ndio msanii wa hiphop kutoka pwani ambaye atatamba zaidi. Donrich amesema
ya kwamba ana imani kubwa sana na ushairi wake na style yake kwani
anaongea vitu ambavyo vipo mitaani na ni mambo ambayo kila mtu anaweza
ku,relate nayo. Akitoa mfano wa wimbo wake mpya ambao amezungumzia
jinsi alivyoishi vizuri na kukubalika kuliko hapo awali kwa sababu
mafanikio ameyapata na maisha yanamuendea vizuri.
‘’Nilipokua
jana sipo nilipo leo na naamini kila mtu hua ana ndoto ya kupata
mafanikio ili mbeleni asiwe kama alivyokua awali. Ni kitu ambacho kila
mtu anaweza ku,relate nacho. ‘ Donrich amesema
hayo huku akisistiza ya kwamba yeye ndio msanii wa hiphop pekee wa
kuangaliwa mwaka huu wakati alipokua anachia track yake mpya ambayo
unaweza kuipata >>HAPA
Comments
Post a Comment