Wynas Aachana Na TeeHits Na Kujiunga Na Record Label Mpya
Nilimuorodhesha kama mmoja ya wasanii ambao huenda wakapasua mbarika sana mwaka huu wa 2017 >>HAPA. Hitmaker wa KITORIRO, Wynas ambaye amekua yupo chini ya uangalizi wa TeeHits inayomilikiwa na Producer Tee ameihama label hio na kujiunga na label nyengine.
Wynas ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliachia wimbo wake wa NARINGA amejiunga rasmi na BigDreams ambayo ndio label inayomuangalia msanii Kush Tracey. 'Nimejiunga na BigDreams kwa sababu nimeona ni kampuni ambayo ina nia na uwezo wa kufanikisha ndoto zangu. Namshkuru sana Producer Tee kwa sababu amenitoa mbali na kunifikisha nilipo kwa sasa kwa sababu amekua kama mzazi kwangu ila lazima mtu apige hatua asonge mbele. Kulingana na ile mikakati tuliyopanga na BigDreams niko na imini sana ya kwamba tutafanikisha.' Wynas ameeleza akithibithisha habari hizo.
'Wynas ni msanii ambaye ana,talent kubwa sana. Nimekua nikimfuatilia kwa mda mrefu sana na nliona ya kwamba nikimshika mkono tunaweza kufanya vitu vikubwa sana. Ndio mwaka umeanza so ni kufanya kazi tu kwa sana kwa sababu tushaanza kutayarisha kazi na tutaachia karibuni.' Ricky Bekko ambaye ndio mmilikiwa BigDreams amesema huku akiongezea ya kwamba akiwa BigDreams, producer wake rasmi atakua producer anayesifika kwa utayarishaji wa mziki, P Lion ambaye amehusika kutengeneza hits kadha na wasanii kama vile Twenty 2, SudiBoy na wengine wengi.
Comments
Post a Comment