ThrowBack Track... Totti & Sleem G Feat. Gates Mgenge- JUU JUU
Mwaki ni 2012 ambapo Producer Totti japo alikua tayari ashaonyesha uwezo wake wa kutayarisha mziki kupitia hits kama vile 'Maria' ya Ali B na Nyota Ndogo alikua hajazoeleka sana kama msanii. Wakati huu ndio pia alikua ameshirikiana na wasanii kadhaa kama vile Johnny skani, K-lama,Kavalier na wasanii wengine katika wimbo wa We Run M.S.A na collabo nyengine na Kidis katika wimbo 'Tujirushe'.
Wakati huu pia Sleem G naye ndio alikua anafanya solo projects zake baada ya kuvunjika kwa kundi lao la Outta Limits huku mtangazaji Gates Mgenge naye alikua anatamba na kipindi chake cha 'MashavMashav' akiwa na mtangazaji mkongwe Donde Samora huku akiwa anatamba katika viwanja vya burudani kama Dj, hypeman na vilevile MC.
Watatu hao kwa pamoja waliingia studio na kufanya track kwa jina JUU JUU, japo haikua wahi kuhit sana ila ilipata kuchezwa kwa kiasi cha haja katika vituo kadhaa vya redio na kumbi za burudani. Track yenyewe iko >>HAPA

Comments
Post a Comment