Ana Uwezo Wa Kufanya Utake Kunyolewa Ukiangalia Michoro Yake Tu

Akili ni nywele,  kila mtu ana zake na ubunifu na talanta ni vitu ambavyo kila mtu amejaaliwa kivyake.  Uchoraji ni moja ya kipaji ambacho mtu anaweza  akajaaliwa nacho, ila inahitaji ubunifu kutumia kipaji hiki ili mtu kuweza kua tofauti na wengine.
Moses Kituwani, almaaruf  Msanii The Barber ana uwezo wa kufanya michoro kichwani, si kwa kutumia rangi au ‘tattoo’ ila kwa kunyoa nywele ili zitokeee kama mchoro aliobuni au anaotaka anayenyolewa. Kazi hii yake ya usanii wa kuvutia alianza mnamo 2009.
Mwanzoni alikua mchorani stadi ila maisha yakawa hayamuendei vizuri kwa sababu sanaa ya uchorji picha haikua inamlipa vizuri. Ndio ikabidi atafute kazi ambayo itakua inamuingizia mtonyo wa kujikimu na mahitaji yake ya kila siku. Kazi aliyobahatika kupata ilikua ni kua ‘cashier’ katika salon moja mjini Mombasa. Wakati akiendelea na kazi hio alivutiwa na jinsi vinyozi wa pale walivyokua wakinyoa watu kwa style tofauti tofauti na akaanza kujifunza kunyoa.
Kwa ubunifu wake na uzoefu wake wa uchoraji alianza kuchukulia machine ya kunyolea kama kalamu ya uchoraji ndio akaanza kufanya michoro kwa wateja wake ambao walitokea kupenda style zake za michoro sana. Urebeshaji wake na ujuzi wake wa kunyoa si mcheo ndio maana mwishoni mwa mwaka jana Msanii The Barber aliweza kupata  tuzo  katika shindalo la kitaifa kama  ‘Male Stylist Of The Year’ katika tuzo za AFRO HAIR AWARDS 2016.
‘Sikutarajia kushinda kwa sababu nilikua nashindana na magwiji tajika ila ushindi wangu ulionyesha ya kua nafanya kazi nzuri na inakubalika. Na hakuna kitu kinachopendeza kama kuweza kufurahisha mtu haswaa kama ni mteja umemhudumia alafu uone amependeza na ameridhika.’ Moses ameeleea huku akimalizia ya kwamba bei zake ni za kawaida sana.
Msanii  The Barber anapatikana kupitia 0710 806 233 ( mmicharazio@gmail.com). Facebook- Msanii The Barber na  Instagram  msanii_the_barber. Pia anapatikana Mombasa mjini, katika jengo la Ralli House.  Hizi hapa ni baadhi ya kazi  zake…..


Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele