DJ Ivory Asema Asiwahi Kuhusishwa Tena Katika Tuzo Zozote Za Pwani. Kulikoni?
Mshindi wa tuzo
mbili, Dj Ivory ametangaza
kwambaa hataki tena kuhusishwa katika
tuzo zozote kutoka hapa pwani. Kupitia ukurasa wake wa facebook, Ivory amesema
ya kwamba baada ya kufikiria kwa mda mrefu sasa anaona ni wakati mwafaka wa yeye kusitisha kushiriki katika tuzo zozote kutoka Mombasa na Pwani kwa ujumla
ili kuwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao djs wanaochipuka.
Nikimhoji zaidi baadae, nilimuuliza iwapo kama madai ya
kwamba tuzo za Mombasa/Pwani hua
hazina uwazi wala usawa ndio kumeachangia yeye kufanya maamuzi hayo… ‘ Hapana. Nina imani sana na Awards za hapa
nyuumbani na mimi hua naona ziko fair kabisa ila wale wenye kusema hivyo ni kwa
sababu ya hao kukosa kujiamini.’
Vilevile, Ivory ambaye
ni dj katika kipindi cha MashavMashav,
Pwani FM amesema ya kwamba mwaka huu ni fursa nyingine tena ya kujiendeleza
na kupanua kazi zake kwani kampuni yake ya HHD
Entertainment imepanga kuinua mziki na wasanii wa Mombasa na Pwani kwa
ujumla kwa kiwango kikubwa sana mwaka
huu. Kando na hilo, Ivory amesistiza
ya kwamba mashabiki wake wasiwe na shaka kwa
kudhania ya kwamba ameacha kua dj.
‘Mimi bado ni dj na naamini nazidi
kuboreka kila siku kwa hivyo ma,fans wasiwe na wasi, sijaacha kua dj na
watarajie mambo makubwa sana kutoka kwangu.’
Comments
Post a Comment