Fat S Afichua Kinachomsukuma Kuuza CD Zake Ferry.

Msanii Fat S aka Mtoto Wa Nyanya kwa mda mrefu amekua akiwa kicheko kwa baadhi ya wasanii na  mashabiki kwa kile kinaonekana kama ‘kuhangaika’. Sababu ya yeye kuonekana kuhangaika ni yeye kuonekana mda mwingi akiuza cd za mziki wake katika kivukio cha Likoni.
Japo amekua kicheko na kejeli na kutumika kama mfano ya kua mziki ni mgumu hadi inabidi wasanii wengine wauze cd wenyewe barabarani, kama alivyoimba msanii Chikuzee katika wimbo wa MZIKI alioshirikishwa na Dodo Richy, Fat S hajawahi acha kuuza kazi zake katika kivukio cha Likoni. Hivi ni kwanini? Je ni kwamba hali ni ngumu sana na ndio njia aliyonayo pekee ya kujikimu au mauzo ni vipi?
‘Mimi ferry peke yake pananitosha kufanya biashara na kuendeleza familia yangu. Hata watu wakaungana zaidi ya elfu moja, watasema mpaka wachoke kwa sababu pale ferry ambapo panafanya watu wacheke sana kwa siku pananiingizia karibu Kshs.20,000. Cd moja ni ksh.100. nikiuza cd kidogo kwa siku ni copy 200. Palepale ferry ndio pananifanya najuana na wakubwa, palepale ferry ndio panasomesha watoto wangu na miradi mikubwa ya maana naifanya kwa sababu ya ferry.Fat S amesema huku akisistiza ya kwamba watu wakimuongea na kumcheka yeye kuuza mziki wake ferry hua kunamtia motisha zaidi kwa sababu faida anazozipata katika kivukio hivyo hazina mfano.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele