Brown Mauzo Awahusisha Diamond Na Akothee Katika Video Yake Mpya

Collabo yake na mkali wa bongofleva, msanii AliKiba imemfanya kutambulika pakubwa katika tasnia ya mziki Afrika Mashariki . Nchini  Tanzania, uhusiano wa Brown Mauzo na AliKiba unachukuliwa kama vile wa Harmonize na boss wake Diamond Platnumz, hii ni baada ya AliKiba kutangaza ya kwamba Brown ni mmoja wa wasanii ambao wako katika management yake.

Katika kazi yake mpya Brown ameshangaza wengi baada ya kuachia video ambayo inaonekana ya kwamba amem,copy hasimu wa boss wake, Diamond Platnumz kwa ku,copy idea ya video ya ‘Salome’ ambayo alishirikishwa Rayvanny na vilevile Brown ameipa kazi hio jina la utata (Apotee)  kwani limefanana na msanii Akothee ambaye ana uhusiano wa karibu na Diamond na pia ni mpenzi wa zamani wa Brown. Itazame video yenyewe hapa chini…


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele