Susumila Kufunga Ndoa Mwezi Wa Aprili

Kando na kufanya kazi nyingi na kubwa mwaka wa 2016, moja ya vitu vilivyoongelewa sana kumhusu ni kutalakiana na aliyekua mkewe, Kibibi Salim ambaye walikua wameoana kwa miezi 11 tu. 
Miezi  mitano sasa baada ya Susumila kutalakiana na muigizaji Kibibi Salim ambaye walikua wamejaaliwa mtoto mmoja, mdokezi wetu wa kuaminika ametudokezea ya kwamba Susumila anajipanga kufunga pingu za maisha mwezi wa Aprili.
 Mdokeni wetu ambaye ni rafiki wa karibu sana wa msanii huyu amedinda kumfichua  bibi harusi mtarajiwa ila ametudokezea tu ya  kwamba mrembo huyo aliyeteka moyo wa Susumila ni mtoto wa mwanasiasa mmoja tajika kutoka eneo la pwani na harusi ya wawili hao haitafanyika nchini Kenya. ‘Zile safari nyingi ambazo Susumila amekua akisafiri zimekua si za matembezi tu bali ni za matayarisho ya harusi yao. Harusi yenyewe imepangwa kuhudhuriwa na watu 35  tu. Watu wote hao watagharamiwa usafiri na malazi kkatika nchi ambayo kutafanyika harusi hio.’ Mdokezi wetu ametueleza. Nilipomtafuta Susumila kuthibithisha uvumi huu alinijibu tu kwa kicheko na kukataa kufunguka.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele