Je, PiliPili FM ‘Walimkanyagia’ Interview Akothee?


Siku moja kabla ya tamasha lake la ‘pre valentine’ msanii anayeaminiwa kua msanii tajiri zaidi nchini Kenya, Akothee alikua anastahili kuwa na mahojiano katika kituo cha redio cha PiliPili FM katika kipindi cha MwakeMwake Live na mtangazaji Gates Mgenge ila inasemekana ya kwamba msanii huyo alikatazwa kuingia katika studio za PiliPili FM hata baada ya kufika katika  kituo hicho cha redio. Je ni kipi kilichosababisha msanii huyo kutohojiwa hata baada ya kufika PiliPili FM?

Kulingana na producer wa kipindi hichho, Clavery Khonde ni kwamba mahojiano yalikua yamepangwa kufanyika kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa moja jioni, tamati mwa kipindi hicho lkini msanii huyo akafika dakika tano kabla kipindi hicho kuisha… ‘Si kwamba Akothee aliringiwa au alibaniwa lakini ni kwa sababu alikuja kuchelewa na ilikua vigumu kufanya mahojiano. Alikuja dakika tano kabla kipindi kuisha na kulingana na sheriia ya kituo  huo ndio mda ambao mtangazaji hu,signout.’
‘Akothee ni msanii mkubwa na anahitaji mda mwingi katika mahojiano na ukizingatia uchangamfu wake hauwezi kumpa dakika tano tu. Tulimueleza manager wak kuhusu timing za ku,sign out na akaelewa so hakuna mvutano wowote na tutapanga kufanya mahojiano hayo siku nyingine.’ Gates Mgenge aliongezea.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele