Nimetungia Wasanii Wengi Hit Songs Bila Kuitisha Hata Senti - Producer AMZ

Producer mkali na mkongwe kutoka studio za Tempoz, Amz wa Leo amejipiga kifua katika swala zima la uandishi na kusema kwamba sio katika upishi wa beat tu pekee bali hata katika swala zima la utunzi yuko vizuri saana. Kulingana na Amz ni kwamba ameshawahi kutunga hits nyingi sana ambazo zimewaacha mdomo wazi wasanii wenyewe anaowaandikia.


"Nina uwezo wa kukuandikia wimbo hadi ujiulize nilichokifikiria ni kipi na wazo la wimbo limetokea wapi.” Amz amesema kuwa kuna hits nyingi kubwa zilizo na mkono wake ila hajalipisha hata senti.
"Nikijiskia kuandikia mtu naandika tu bila kutarajia malipo wala credits zozote. Hua ni hisia fulani hunijia na hunisumbua mpaka hujipata nimepigia msanii yeyote simu aje nimuandikie wimbo ndio nijiskie sawa....." Amz amesema huku akidinda kutaja baadhi ya ngoma ambazo zina utunzi wake.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele