Pastor Aeleza Kwanini Alim'beba Mgongoni Kalonzo Musyoka
Kuanzia siku ya Jumapili, picha ya aliyewahi kua makamu wa
rais, Kalonzo Musyoka akiwa amebebwa
mgongoni na pastor flani ilizua gumzo sana katika mitandao ya kijamii. Haikua
imebainika ni kwanini walifanya kitendo kile na ilikuaje mpaka ikafikia pale.
Siku ya Jumatatu, katika kipindi cha MegaBreakfast, Baraka FM, watangazaji Billy Miya na Diana Tangut
aka Presenter 001 waliweza kumtafuta
pastor huyo, Pastor Daniel Idaturi wa Jesus
Winning Soul Ministry ili aeleze haswaa kilichokua kinatendeka katika picha
ile.
‘Katika kuhubiri
nilikua nahubiri pale Yesu Kristo
alipoagiza mwanafunzi wake amlee punda na kumwambia ya kkwamba atakapoulizwa ni
nani anayehitaji punda yule basi asema ni Bwana wangu ndiye anayetaka punda. Kalonzo Musyoka alikua Yesu na mimi nikawa
Punda.’ Pastor Daniel
alieleza. Je alipoamriwa kumpanda pastor
mgongoni, Kalonzo aliipokeaje amri hio? Ni waumini ndio walimshabikia kumpata
pastor au ilikuaje? Na je ni kweli baada ya ibada pastor Daniel alipewa donge nono na Kalonzo
Musyoka? Jua majibu ya maswali hayo
na usikilize mahojiano hayo kwa kubonyeza >>HAPA
Makubwa!!
ReplyDelete