Baada Ya Kufumaniwa Na Mke Wa Waziri, Ajitoa Mafichoni Kwa Mara Ya Kwanza Na Kueleza Yaliyotokea



Mwaka wa 2015, Profesa Nasha alikua mmoja wa wasanii ambao walikua wanafanya vizuri kutoka eneo la pwani.  Wimbo wake wa POLE ulikua unachezwa sana katika vituo vya redio na ilipofika Januari 2016, Nasha  akaachia wimbo mpya kwa jina MOTOKAA  ambao alikua amekamilisha kutayarisha video yake akisubiri  muongozaji amalize editing ndio aiachie baadae.
Alichokua hajui ni kwamba video hio ingekwama na maisha yake kubadilika kwani alipatikana na mkosi ambao nusura auliwe. Profesa Nasha alifumaniwa akiwa na bibi ya waziri mmoja katika serikali ya  Kenya. Ni tukio ambalo lilimuacha na majeraha mabaya sana kwani aliangukia kipigo cha mbwa kutoka kwa walinzi wa waziri huyo na alipopata nafasi alitoroka, si hotelini mle tu bali ilibadilisha makao na kuenda mafichoni.
‘Kusema ukweli mimi sikuwahi kujua kua Yule alikua bibi ya mtu kwa sababu hakuwahi kuniambia. Tukio la kufumaniwa halikua rahisi kwangu kwani sikupewa nafasi ya kujieleza na nilipopata nafasi nilikimbia na kuamua kuenda mafichoni kabisa kwani nilijua kilichofuata ni kuuliwa tu. Mimi kuenda mafichoni hakukuniathiri kimziki tu bali hata kimaisha kwa sababu hata kazi niliyokua nafanya ilinibidi niiache kwa kuhofia maisha yangu. Lakini yote hayo yamepitwa na wakati na sasa nimerudi kuendelea kutooka pale nilipokua nimeacha. Kuna kazi nilikua nimefanya na Khaligraph Jones na nyengine   nilifanya na Otile Brown ila hizo zitasubiri kidogo na kwa sasa naachia video ya wimbo wa MOTOKAA.' Nasha amesema Video yenyewe ambayo ilicheleweshwa na fumanizi la msanii huyo hii hapa chini…..

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele