Berry Black Awakashif Mashabiki, Wasanii Na Washikadau Wa Mziki Pwani
Ni mmoja kati ya wasanii kutoka nchini Tanzania ambao
wameweza kujulikana sana Afrika Mashariki. Akiwa na mwenzake Berry White wakiwa na kundi lao la 2Berry, walihit sana na wimbo NATAKA KUA NAWE ambao ulitayarishwa na Producer Shirko ambaye ni producer kutoka Mombasa. Kufanya
kazi kwa wawili hao hakukuishi hapo kwani karibu ntimbo zote za Berry Black zimeandaliwa na Producer
Shirko ambaye ndiye producer anayetayarisha nyimbo za Yamoto Band.
Hapo jana, usiku wa Alhamisi, katika ukumbi wa Dans Lounge, katika tamasha la Celebrity Thursday, Berry Black
aliwatolewa mapovu na kuwakashif mashabiki kutoka Mombasa
na washikadau katika sanaa ya mziki kutoka Mombasa kwa kukosa ku,support watu na kazi za nyumbani. ‘Nyinyi watu wa Mombasa
ham,support watu wenu. Shirko
alipokua anaongea hapa hamkua munampigia makofi lakini mimi nimeshika mic
munanipigia makofi. Hizo nyimbo munazo zishabikia na kuniambia niimbe yeye ndio
amezitengeneza. Yamoto Band kufika
walipofika ni mkono wa Shirko. Wimbo
wa P Square na Diamond, ni Shirko ndio
ametengeneza. Musiwe hivyo, shabikieni wa kwenu.’ Msanii huyo alisema huku akionekana kujawa na
hasira.
‘Kule
kwetu ukiskia Wema yuko na hili
utaona mashabiki wanajitokeza kumuunga mkono. Diamond akiwa na hilo, mashabiki wanamuunga mkono lakini
nawashangaa watu wa Mombasa. Hivi
hakuna hata msanii wa Mombasa
aliyemfuata Shirko ili kufanya kazi
naye wakati mnajua ya kwamba anafanya kazi nzuri. Mimi nimeinuliwa na Shirko. Yamoto wameinuliwa na Shirko hadi kufika pale walipofika.
Badilikeni. Mombasa hamtaendelea kama hama,support na kupenda watu wa nyumbani.’’Berry Black alimalizia.
Hapo ni kweli kabisa!! Pwani tuna shida sana yani hata show ya bure ya msanii wa hapa pia watu hawaendi kusupport.inakera sana
ReplyDeleteKaongea kweli...
ReplyDelete