Hiki Ndicho Kitakachotokea Katika Kivukio Cha Mtongwe Kuanzia Ijumaa Hii
Shirika la huduma za ferry limetangaza ya kwamba kivukio cha
Mtongwe kitaanza kutumika tena
kuanzia siku ya Ijumaa , Februari 24.
Kuanza kutumika tena kwa kivukio hicho cha Mtongwe kutaleta afueni kwa zaidi ya
abiria 30,000 kila siku. Kivukio cha Mtongwe
kitaanza tena huduma zake baada ya
kufanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi milioni 6 baada ya serikali
kuondoa ferry mbili zilizokua zikihudumu katika kivukio hicho mnamo 2012.
Msimamizi mkuu kwa huduma za ferry, Bakari Gowa ameeleza ya kwamba
moja kati ya ferry tano zinazotumika katika kivukio cha Likoni itatumika
katika kivukio hicho cha Mtongwe. ‘Moja kati ya MV LIKONI na MV KWALE
itakua inahudumu katika kivukio cha Mtongwe.
Kwa kuanzia, huduma za ferry Mtongwe zitakua wakati wa msongamano, alafu ratiba
ya huduma itabadilika kulingana na jinsi huduma hizo zitakavyopokelewa na
huenda zikaanza kufanya kazi siku nzima.’
Bwana Gowa ameeleza huku akiendelea na kusema ya kwamba anaamini
ya kwamba kurudi kwa huduma hizo kutakua kwa manufaa kwa wakaazi wa Mtongwe
na watumizi wa kivukio hicho ikiwa ni
moja wapo ya mikakati ya kupunguza msongamano katika kivukio cha Likoni.
Itakumbukwa ya kwamba April,
29 mwaka wa 1994, takriban abiria 272
walipoteza maisha yao baada ya ferry kuzama katika kivukio hicho, tukio ambalo
linaorodheshwa kua ajali kubwa ya baharini nchini Kenya. Kufikia mwaka wa 2005,
takriban familia 81 zilikua
zimepokea fidia ya jumla ya Kshs
36,902,472.
Sawa sawa kabisa
ReplyDelete