Baada Ya Mziki Ni Majanga, Kaa La Moto Naye Aibuka Na MZIKI NI MATANGA

Kaa La Moto naye ameibuka na wimbo alioshirikiana na Young Njita pamoja na mwanadada Wandia ambao wameonekana ni kana kwamba wanaunga mkono kauli ya Dogo Richy ya kwamba sanaa ya mziki katika eneo la Pwani limejaa shida na changamoto nyingi tu.
Mziki umekua matanga wengi hatuna huzuni, hatuna uhuru labda Raila na Kibaki show hawakupi na wakikupa hawakulipi...uliza Sango mjini mipango labda wa kando wanagonja tufe waje kuleta michango…  ni baadhi ya mashairi ya wimbo huo ambao umeandaliwa video kali sanana director mashuhuri kutoka mjini Malindi, Marvin Y. Brudas. Ni video ambayo imetayarishwa katika mandhari tofauti na mazoea ya video zingine za kizazi kipya kwani ilitayarishwa katika jangwa na ubunifu mzuri wa maigiuzo. Itazame video hio ya mkali huyo wa hiphop katika Afrika Mashariki aliyomshirikisha Young Njita ambaye anaonekana kuteka na kutawala soko la katika kaunti ya Kilifi.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele