CHIKUZEE AUNDA KUNDI LA MZIKI
Msanii Chikuzee ni mmoja kati ya wasanii tajika kutoka kanda
ya pwani ya Kenya. Waakati alipoachia collabo mbili na msanii Susumila
mashabiki wengi walitamani sana wawili hao waungane na kuwa kundi moja ila
uhusiano wao haukuduma sana kuanzia 2015 wawili hao walianz kua na tofauti
baina yao.
CNew naye alikua pamoja na msanii Fat S na
35% katika kundi lao la RBeez, enzi hizo CNew alikua akijiita
Njemba Boy. Pia nalo ni kundi ambalo
lilikuja vunjika baadae. Miaka imesonga sasa na wawili hao, Chikuzee na CNew
katika siku za hivi karibuni wameonekana wakiwa na ukaribu sana na wameweka
wazi ya kwamba, pamoja na Producer B.I wamekuja pamoja na kuunda kundi kwa jina
DOSSARI INTERNATIONAL.
‘Tumeunda kundi na mtindo wetu wa mziki unaitwa TamTam
Flevaz. Si kwamba ni kundi ambalo linatufunga sana bali kila mtu bado ana uhuru
wa kufanya solo projects zake lakini tukiwa pamoja ndio Dossari International.
Kuna kazi nyingi ambazo tayari tushazikamilisha
nay a kwanza ndio yumeiachia hivi sasa na inaitwa DUNIA NZIMA.’ CNew
ameeleza hayo huku akiahidi mashabiki wangojee kazi nyingi nzuri kutoka kwao kwani anaamini huu mwaka ni wakati wa kundi
hilo kutamba. Itazame video ya kundi hilo ambalo linatarajiwa kuteka nyoyo za
wengi mwaka huu hapa chini….



Comments
Post a Comment