Azidisha Mbwembwe Baada Ya Kutoka Mafichoni
Ni mwezi jana tu ndio msanii Professa Nasha aliweza kuachia
kazi yake mpya baada ya kua mafichoni kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja
baada ya kufumaniwa na mke wa mwanasiasa maarufu hapa pwani. Stori hio iko >> HAPA.
Baada ya kurudi rasmi katika mziki, Professa Nasha ameamua ni kazi baada ya kazi kwani baada ya mwezi
tu tayari ameandaa video mpya. ‘Nilikua nimewamiss mashabiki wangu na najua
walikua wanakosa sana kazi nzuri kutoka kwangu lakini hio ni zamani kwa sababu
nimerudi kuwaridhisha na nawaahidi kuwapa kazi nzuri bila kuchoka. Naelewa ya kwamba si rahisi kurudi nilipokua baada ya kimya cha mwaka mmoja lakini najibidisha kwa ajili ya mashabiki wangu.’ Nasha
amesema hayo wakati alipokua anazindua video yake mpya ya ULIENDA WAPI iliyoandaliwa na DreamLand Music. Kua wa kwanza kuitanza video hiyo hapa chini....
Comments
Post a Comment