Fat S Afunguka Kuhusu Mziki, Kuuza CD, Mayai Na Diss Ya Dogo Richie
Wiki hii msanii Fat S
ameongelewa sana baada ya kusemekana ya kwamba katika siku za hivi karibuni
amekua akionekana akiuza mayai katika kivukio cha Likoni.
Kelvin Jilani / Mtu
Bei alifanikiwa kumpata Fat S na
wakawa na mahojiano ambayo Fast S
alifunguka mengi kuhusu yeye mziki na biashara zake. Katika mahojiano
hayo, Fat S alifunguka na kueleza ni jinsi gani amekua akiifanya biashara
yake ya kuuza CD pale Ferry na inamuingizia pesa kiwango gani.
‘Unajua mimi ni
msanii na mimi ni kioo cha jamii. Kila
kitu ninachofanya hua nafanya kwa ajili ya kufunza jamii, kwa hio ple ninapo
uza Cd ferry naonyesha jamii ya kwamba nategemea kazi yangu na kipaji change
ndio kinanilipa. Mimi sifanyi mziki
ubishow bali nafanya kama biashara. ‘ Fat
S amesema huku akisema ya kwamba wale wasanii wengi ambao wamekua
wakimcheka ndio ambao hawana lolote kwani ni njaa na kukosa pesa ndio wanajua
‘Msanii
anayejua analofanya hawezi akaingia studio na kutoa pesa zake akaimba watu. Dogo
Richie alijua kuna wasanii vigogo ndio akaamua kuwataja
ili apate kiki. Dogo Richie amepata umaarufu kwa kuwaimba wenzake ila asilojua ni kwamba amejijengea chuki.’ Fat S
amefunguka. Je ana beef na Dogo Richie kwa kumuimba katika nyimbo mbili kama mfano
wa jinsi mziki unavyohangaisha wasanii?
Na vipi kuhusu yeye kuuza mayai katika kivukio cha Likoni? Msikilize
alichokisema kuhusu hilo >> HAPA
Comments
Post a Comment