Otile Brown Aeleza Kwa Hasira Kilichompelekea Kujitoa DreamLand Music

Katika mda wa wiki mbili sasa, msanii Otile Brown amekua akigonga vichwa vyaa habari baada ya kubainika ya kwamba kumekua na ugomvi kati yake na manager wake Dr Eddie baada ya Eddie kuzitoa video zote za msaniii huyo katika mtandao wa Youtube.
Na hapo  jana asubui, Otile Brown aliweza kutangaza rasmi kupitia mitandao ya kijamii ya kwamba amejitoa katika management hio. Kasssim Mbui wa PiliPili FM alifanikiwa kufanya mahojiano na msanii huyo ili kujua ni kipi haswaa kilichojiri hadi kupelekea msanii huyo kufanya maamuzi hayo.
‘Nimekua nikitumia pesa zangu kuji,market kazi zangu. Kuna vitu alikua anastahili afanye lakini hakua akifanya. Alikua anafaa anilipie nyumba lakini nilikua najilipia mwenyewe. Baada ya ugomvi nlimtafuta tusuluhishe lakini amekua akikata simu zangu na kutoshika. Nimejaribu kumpigia zaidi ya mara mia mbili. Upande wa hela kuna mkataba kila mtu ana kile anachochangia na kila mtu ana asilimia yake ya mgao ambayo anapaswa kupata kipato kinachoingia.Hauwezi sisitiza kusema ya kwamba unataka upate mgao wako kamili wakati hautimizi majukumu yako kamili.Otile amefunguka hayo huku akisema mengi zaidi yaliyoibuka kadi ya wawili hao hadi kufikia kufanya maamuzi hayo.
Sikiliza mahojiano hayo aliyofunguka kwa kina kwa kubonyeza >>HAPA

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele