Kundi Linalojihusisha Na Mziki, Uhamasisho na Biashara Kwa Vijana
NewLife Music si
kundi tu la mziki bali pia ni shirika linalojihusisha kuhamasisha vijana kuishi
maisha yenye muelekeo katika jamii.
Waanzilishi wa kundi hili, Kally D na Baracka J.O hawafanyi
mziki wa injili tu ila wanahubiri amani haswaa wakati huu nchi inapoelekea
kufanya uchaguzi. Katika kuhubiri kwao, wanaowalenga sana ni vijana kwani hao
ndio hutumika sanasana na wanasiasa na bila uhamasisho mzuri husababisha
madhara makubwa si kwa vijana wenyewe tu bali kwa nchi nzima kwa ujumla.
‘Kimziki kwa sasa Kally
D ameachia video yake ya NISHIKE na
inaendelea kufanya vizuri na kuanzia
mwezi ujao tutakua tunatayarisha video ya wimbo mmoja wangu.’ Ameeleza Baracka J.O ambaye ameendelea kusema ya kwamba wanajihusisha na
biashara ya mavazi na wako na clothingline
( New Life Music - NLM) ambayo wanaipangia kuifanyia uzinduzi
mkubwa hivi karibuni.
‘Tunakaribisha wasanii wenzetu wa injili
wajiunge nasi. Atakayetuma maombi atakaguliwa kulingana na utaratibu wa panel
inayoongozwa nab boss Bizzoh na iwapo mtu atapitishwa basi atajiunga nasi na
kufanya kazi nasi.’ Amemalizia Kally D.
Comments
Post a Comment