Hiki Ndicho Alichokifanya Baada Ya Kutimuliwa Studio
Angekua na moyo mwepesi basi hata tusingewahi kumsika
kwani kilichomtokea katika jaribio lake
la kwanza kufanya mziki kingemkatisha tama ila kwa kua alikua na malengo ya juu
hakutetereka ila aliogeza ujasiri na moyo zaidi wa kufikia malengo yake.
Adily Tozy alianze kupenda mziki tangia akiwa mtoto. Miaka
miwili iliyopita Adily ndipo alipoona ya kwamba wakati mwafaka wa kuanza mziki
rasmi umewadia. Akajizoazoa akiwa amejihami na mashairi kuenda studio afanye
mawili matatu. Baada ya kupitishwa huku na kule kwa mda kiasi hatimaye alionana
na producer ambaye alimuandalia beat ya
wimbo na kumpa akajitayarishe kurekodi.
Alirudi studio baada ya wiki mbili na akabaahatika kupata
mda mzuri na producer wake. Baada ya kuwa studio kwa zaidi ya takrriban masaa mawili
wakijaribu kuandaa wiimbo wake wa kwanza, producer aliona ya kwamba msanii huyo
likua hawezi kabisa na akaamua kumtoa nje ya studio na kumrudishia pesa zake na
kumwambia asiwahi kurudi tena katika
studio hio na ushauri anaoweza kumpa ni kwamba aachhe mziki na pesa alizokua
atumie katika mziki basi aende akaekeza katika biashara nyengine ila sio katika
mziki kwani hio talanta haya.
Alikata tama ila hakufa moyo kwani aliamua ya
kwamba atafanya mazoezi zaidi. Baada ya miaka miwili alijipiga moyo konde na
kufunga safari tena na kuenda katika studio za Neptune Records ambako chini ya
usmamizi wa producer Lameck aliweza kufanya track ambayo mda wa kwanza aliweza
kumtumia kwa njia ya whatsapp alikua producer aliyemfukuza studio awali. Pindi tu alipoisikiiliza alimpigia simu na
kumuomba msamaha na kumwambia awe akienda studioni tena na atakua anamfanyia
mziki bila malipo yoyote. Wimbo huo ambao umekua ukimzolea sifa kila
atakapoutambulisha uko hapa >>HAPA
Comments
Post a Comment