SUSUMILA ANA LIPI TENA?
Msanii anayetamba kwa sasa na wimbo unaokwenda kwa jina
IHALE Susumila yusuf anategemea kuiachia video ya wimbo huo(ihale) tarehe 25
mwezi huu wa mei.Akiongea na
machampaliblogspot.com,msanii huyo amesema kuwa video hiyo ambayo iliongozwa na Ricky becko iko katika hatua za
mwisho kumaliziwa na amewataka mashabiki
wake watarajie video nzuri kutoka kwake.Susumila pia amefunguka na kusema kuwa
mashabiki wake watazamie kazi nyingi saana mwaka huu kutoka kwake zikiwemo pia za
kushirikishwa ambapo moja wapo ni video ya wimbo alioshirikishwa na busy k unaokwenda
kwa jina la kimwana itakayoanza kutayarishwa baada tu ya video ya ihale kutoka.Kwa
sasa susumila anazidi kupeta na single yake ya IHALE
pamoja na nyimbo kadhaa alizoshirikishwa kama vile KIDEKIDE aliyoshirikishwa na
dazlah na KIMWANA aliyoshirikishwa na busy k.
Comments
Post a Comment