MSIKILIZE KAVALIER AKIZUNGUMZIA MZIKI WA PWANI

Kwa kiwango kikubwa kwa sasa mziki wa pwani tunaweza kusema kuwa umepiga hatua tofauti na wakati wa siku za nyuma.Katika kiwango cha sasa kila mmoja anazidi kupambana kufika katika viwango vya juu binafsi na pia kuupeleka mziki wa pwani kiujumla katika viwango vipya kitaifa na hata kimataifa.Kwa upande wake msanii Kavalier ambae kwa sasa anatamba na kibao kwa jina memsoza amefunguka na kusema kuwa kwa sasa kinachohitajika katika mziki wa pwani ni ubunifu.Akizungumza na Mp Kelvin Jilani wa Sifa f.m ,Kavalier amesema kinachoiponza sanaa ya pwani ni idadi kubwa ya wasanii kuigiza mitindo ya kigeni haswa kutoka mataifa ya magharibi ya dunia na magharibi ya Afrika hususan Nigeria na Ghana hivyo basi kuinyima sanaa  ubunifu na utofauti.Msanii huyu ametilia shaka hali hii akisema endapo wasanii wa pwani wangependa kutoboa mipaka na kupeta katika mziki kiujumla wanafaa kubuni mtindo tofauti ambao utakua mgeni kwa maskio ya watu wa nnje ya pwani.kwa mengi zaidi huyu hapa msikilize akifunguka mengi ikiwemo swala la beef baina ya wasanii haswa katika sanaa ya pwani..
                                                        LISTEN HERE

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele