ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele
Ukitaja wasanii ambao waliwahi kutamba kutoka eneo la pwani huwezi kukosa kumtaja Daddy Sele . Miaka ile ya 2008 alikua anatamba sana na wimbo wake wa Machungu na Ananipenda , wimbo ambao aliufanya na Fat S . Wimbo wake wa Machungu , uliotayarishwa BC International ndio single yake kubwa ambayo ilimfanya atese sana katika anga za mziki baada ya kufanya track kama vile Badman , aliyokua ameifanya katika studio za Tabasamu Records ambayo haikuwahi kupata airplay nzuri. Kwa sasa, Daddy Sele ameacha kabisa mziki na kulingana na yeye ni kwamba yeye kufanya mziki basi itakua ni miujiza, aliongelea hilo >> HAPA. Kila siku ya alhamisi utakua unapata fursa ya kupata wimbo/video moja ya kitamboooo... unaweza ku,request katika eneo la ku,comment hapo chini. Download/Listen MACHUNGU >> HAPA
Comments
Post a Comment