NEW VIDEO: Susumila Feat Kush Tracey-UMENITOSHA

Ni kitu kizuri kuona kwamba siku hizi wanamziki wengi wa pwani wameamua kuukumbatia ubunifu na vile vile kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa kuanzia katika utayarishaji wa nyimbo hadi video za muziki.Hii ni hali inayoamsha matumaini makubwa katika safari ya ukuaji wa muziki wa pwani.

Ukweli wa msemo wa pafukapo moshi pana moto unadhihirika wazi hapa, kwani Ikiwa ni masaa machache tu baada ya msanii SUSUMILA aachie ngoma yake mpya UMENITOSHA aliyomshirikisha KUSH TRACEY,msanii huyo tayari ameachia video ya ngoma hiyo.

Kipya na kigeni katika Video hii iliyofanywa na muongozaji RICKY BECKO wa CLICK MEDIA GROUP, Nairobi ni kwamba video hii imefanywa kwa mtindo wa ANIMATION hivyo basi kumfanya SUSUMILA kuwa msanii wa kwanza kutoka Pwani kufanya ANIMATION VIDEO
ITAZAME 

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele