Je mfumo wa mziki wa makundi unaanza kuiteka Mombasa?
Inaonekana kuwa mfumo wa makundi unaanza kuchukua pamoja na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.Kama umechunguza,haihitaji umakini kuona mafanikio ya kundi la tanzania maarufu kama YAMOTO BAND.Mafanikio ambayo kundi hili limeandikisha tangu kubuniwa kwake ni makubwa kufikia kiwango cha makundi mapya kubuniwa kama vile RUBEEZ BAND ambayo kiujumla pia yamefanya vizuri.
Inaonekana wasanii wa hapa mombasa wamechukua muamko wa mfumo huu, na kuanza kujikusanya makundi ya wasanii wenye vipaji ili kuunda makundi mfano wa YAMOTO BAND ili kuleta mapinduzi katika mziki wa mombasa.
wasojali band
Mfano mzuri ni kundi kama vile WASOJALI BAND lililoko chinini ya mikono ya PRODUCER NOIZER wa GREENHOUSE RECORDS. Kundi lingine changa linalokuja kwa kasi ya juu saana lijulikanalo kama NUMBER ONE ACADEMIA.
Hili ni kundi ambalo linawajumuisha SUDIBOY, CHAPATIZO (TIZZOH), SHEMBWANA MASAUTI na KIGOTO M'MBONDE. Ni kundi ambalo liko katika mikono ya Producer TK2 wa NUMBER ONE RECORDS. Hii hapa kazi yao ya kwanza
BONYEZA HAPA KU,DOWNLOAD/KUSKIZA
Comments
Post a Comment