Tulielewana kufanya collabo na Diamond Platnumz lakini ananichezea mchezo wa "paka mshike panya"-D'BANJI. Diamond pia ajieleza


Kokomaster au ukipenda muite D'Banji amelalamika akisema kwamba walipokutana na Diamond walielewana kwamba watafanya collabo lakini Diamond amekua akimpiga chenga.
D'Banji ambaye alitwaa tuzi la 'MAMA Evolution' katika tuzo za MAMA 2015, alisema ana imani ya kwamba kabla mwaka muishe watakua tayari washafanya collabo hio.
Diamond naye alieleza ni kwanini amekua akizingua kufanya collabo na D'Banji.

 “Tulikutana kule kwenye 'Do Agric' tukafanya Cocoa na Chocolate, tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa ngazi kwa ngazi kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza kufanya na yeye ya kwanza.” alisema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Comments

Popular posts from this blog

ThrowBackTrack.... MACHUNGU - Daddy Sele